Na Sophia Kingimali
Katika kuhakikisha teknolojia inakua hasa katika sekta ya utalii kampuni ya GOHERE Tanzania imekuja na huduma ya kutafuta hotel na vivutio kwa kutumia simu janja.
Akizungumzia huduma hiyo jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho yanayoendelea mlimani city Mkurugenzi mkuu na muanzilishi wa kampuni hiyo Menno Biesiot amesema kufuatia filamu ya Royal tower iliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndio imevutia zaidi wao kuja kuwekeza Tanzania.
Amesema kumekua na ongezeko kubwa la watalii nchini hivyo kwa kutumia huduma hiyo(application)itasaidia mtalii anapokuja nchini kuweka oda(booking)ya hotel atakayofikia pia na sehem atakazotembelea.
“Hii Application ni njia rahisi ya mtalii kutumia pindi anapotaka kuja nchini itamsaidia kujua hotel zilizopo sehemu anayotaka kwenda lakini pia gharama na mambo mengi hii itasaidia kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia kwa maana amesaidia sana kutangaza utalii wa hii nchi”amesema Biesiot
Kwa upande wake Meneja mwajili kutoka kampuni hiyo Winfrida Msabuni amesema kampuni hiyo imejidhatiti kutoa huduma nchini kwa kuvutia watalii wengi kwani hiyo imekua njia rahisi na ya haraka.
“Hii kampuni ipo sehemu mbalimbali duniani na imekua ikifanya vizuri kuanzishwa kwa huduma hii nchini kutasaidia kuzidi kuvutia watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani hii kwetu Tanzania hivyo nitoe rai kwa watu kuitumia.