Na Sophia Kingimali
Mkurugenzi wa Kili mediAir Dkt Hussein Abradha ameipongeza serkali ya awamu wa sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fursa kwa vijana na kuitangaza nchi na kuvutia uwekezaji.
Haya ameyasema Mkurugenzi huyo wakati alipokuwa akizungumza na FULLSHANGWE kwenye maonyesho ya saba ya Swahili ya kimataifa ya utalii yanayoendelea katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam.
Amesema wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na serikali katika kuhakikisha watalii wanaotembelea vivutio wanakua salama kwani wao wamejipanga vizuri katika kuhakikisha Afya za watalii pindi wanapokuwa kwenye vivutio zinakuwa salama.
“KilimediAir tumejipanga kuhakikisha utalii wetu unazidi kupamba moto nchini kwani nchi yetu ipo salama na sisi tumejipanga vizuri katika kuhakikisha usalama wa mtalii lakini pia afya yake na majanga yoyote ambayo anaweza kuyapata pindi anapokuwa kwenye vivutio vyetu”
Aidha Dkt Abradha ametoa rai kwa watalii kujitokeza kwa wingi nchini kuja kuangalia vivutio vilivyopo kwani nchi ipo salama na usalama wa mtalii umezingatiwa.
Taasisi ya kilimediAir inajishughulisha na usalama wa watalii katika vivutio na kwa sasa imejikita zaidi Kaskazini huku wakiwa na malengo ya kufikia vivutio vyote nchini pamoja na zanzibar Kwani mpaka sasa imeshanunua vifaa vya kutosha kufanya shughuli hiyo nchi nzima.