Na Sophia Kingimali
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angela Kairuki ametoa rai kwa wananchi kulinda na kutunza maliasili zao kwa ajili ya kukuza na kuendeleza utalii kwa manufaa ya Taifa, vizazi vijavyo.
Hayo amezungumza leo Oktoba 6 jijini Dar es Salaam Waziri huyo wakati akifungua onesho la saba la Kimataifa la Site Swahili Internation Tourism Expo lililohudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema lengo la onesho ni kuendelea na jitihada za kuongeza watalii nchini, katika onesho jumla ya waoneshaji 150 na wanunuzi wa bidhaa 71 kutoka nchi tofauti wameshiriki.
“Viongozi wa mikoa kuendelea kuwa wabunifu katika mikoa yenu na kutangaza vituo vya utalii vilivyopo kwenye mikoa yenu na tunaendelea kukuza utalii maeneo mengine kwasababu tuna maeneo mbalimbali ya utalii, “amesema Kairuki.
Amesema kuwa sekta ya utalii ni muhimu hivyo serikali na wadau wanawajibu wa kuendelea kutangaza vituo vyote vya utalii vya dhamani na vipya nchini.
Amesema serikali inatambua umuhimu wa utalii hivyo wataendelea kuhimarisha miundombinu kama reli na viwanja vya ndege ili kuweka mazingira bora na salama kwa watalii wa ndani na nje.
” Bado tunapenda kueleza kuwa hali ya utalii inakua kwa kasi hivyo lengo ifikapo mwaka 2025 kuwa na watalii milioni tano litafikiwa tunaendelea na juhudi za kuongeza watalii nchini,” amesema.
Aidha amesema wanaendelea kutoa ajira rasmi na zisizo rasmi na utalii makini kuleta watalii.
Naye Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohammed Said amesema katika kuendeleza utalii lazima waboreshe miundombinu na kuondoa tozo zilizo kuw kero kwa wananchi kusababisha kushindwa kufanya utalii wa ndani.
“Pemba tumeanza ujenzi wa kiwanja cha ndege hii itasaidia kuvuta watalii wengi zaidi lakini tunapaswa kuboresha miundombinu yetu ikiwemo ujenzi wa barabara tunatamani kuendesha magari yetu kutoka zanzibar kuja huku kufanya utalii wa ndani lakini kero zimekua nyingi hasa tozo tunapaswa kuliangalia hili.amesema Simai
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale amesema site Swahili Internation Tourism Expo wanatarajia kuwa onesho kubwa Barani Afrika na kuwavutia watalii mbalimbali duniani.
“Onesho hili lilianzishwa mwaka 2019 na hili ni onesho la saba lakini hili ni la tofauti na miaka mingine tunaendelea kuongeza ubunifu na lengo letu ni kuonesha duniani onesho hili,”amesema Mfugale.
Naye,mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia fursa hiyo ya maonyesho kujifunza lakini pia kuonyesha ukarimu na upendo kwa wageni kama ilivyo kawaida.
Sambamba na hayo Chalamila ametoa ombi kwa serikali kufanyia kazi utalii wa mikutano pamoja na utalii wa matibabu(medical tourism)kwa kuandaa documentary nzuri inayoonyesha matibabu yetu nchini ambayo itaweza kuwavutia watalii wengi zaidi.