Serikali ya wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro imekanusha taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu wananchi waliodai kunyanyaswa kwa kuchimbiwa mfereji unaozuia mifugo na wanafunzi Kutoenda Shule kwenye shamba la Mwekezaji la kampuni ya Africa Agro Focus Limited kuwa taarifa hiyo sio ya kweli Bali wafugaji hao ndio waliovamia katika shamba Hilo
Kwa miibu wa taarifa ya Mkuu huyo wa Wilaya, Awali Shamba hili lilimilikiwa na East Africa Sisal Plantation likiwa na ukubwa wa ekari 19,842 kwa hati namba 3917, hati ambayo wakati inatolewa haikuwa na ukomo, Mnamo Julai 1st, 1938 shamba hili lilibadilishwa umiliki, na kumilikishwa kwa Tanzania Sisal Corporation Julai 30, 1968,
Aidha, kulifanyika tena uhamisho kwenda kwa Tanzania Sisal Authority mwaka 1980, kisha mwaka 1998 Mamlaka ya Mkonge Tanzania, ilirudisha sehemu ya shamba hili yenye ukubwa wa ekari 6,795 kwa serikali, na mwaka 2009 serikali ilifanya upya vipimo vya shambahili, ambapo ekari 1,347 zilimikishwa kwa Bodi ya Mkonge Tanzania, kisha bodi hiyo kuuza eneo hili kwa Agro Focus Tanzania ambao ndio wamiliki wa sasa. 28 06:55