Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini -TFRA Happiness Mbele wakati akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akitoa taarifa ya kuelekea maadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 13 Mwaka huu katika Manispaa ya Tabora Mjini Mkoa wa Tabora.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ruzuku kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini -TFRA Louis Kasera (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini -TFRA Happiness Mbele (kulia) wakizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu kuelekea maadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 13 Mwaka huu katika Manispaa ya Tabora Mjini Mkoa wa Tabora.
Meneja wa Kitengo cha Uhusiano, Mawasiliano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini -TFRA Matilda Kasanga akifafanua jambo katika kikao cha Mamlaka hiyo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kuhusu kuelekea maadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 13 Mwaka huu katika Manispaa ya Tabora Mjini Mkoa wa Tabora.
…………………
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini -TFRA imefanikiwa kuongeza upatikanaji wa Mbolea nchini kutoka tani 429,814 kwa Mwaka 2016/17 hadi kufikia tani 1,035,745 katika msimu wa kilimo 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 141.
Pia imeeleza kuwa matumizi ya Mbolea yameongezeka kutoka tani 296,036 mwaka 2016/17 hadi kufikia tani 580,529 Mwaka 2022/23 ikiwa ni ongezeko la asilimia 96.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti TFRA Happiness Mbele wakati akitoa taarifa ya kuelekea maadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 13 Mwaka huu katika Manispaa ya Tabora Mjini Mkoa wa Tabora.
Happiness amesema kuwa lengo la Maadhimisho hayo ni kupanua wigo zaidi wa kuelezea Masuala mbalimbali katika Tasnia ya Mbolea ikiwemo mafanikio yake sambamba na kutoa elimu kwa wadau wa mbolea hususani wakulima na wafanyabiashara.
“Katika maadhimisho yao ya siku ya Mbolea Duniani Kwa Mwaka 2023 nchini Tanzania ni Ajenda 10/30:matumizi sahihi ya Mbolea ya Ruzuku kwa kilimo chenye tija, na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe”amesema Happiness
Aidha Mkurugenzi Huyo wa Huduma za Udhibiti TFRA amesema Kauli mbiu ya Mwaka huu inaendana na jukumu Kuu la Mamlaka hiyo ambalo ni kusimamia ubora wa Mbolea Ili wakulima wapate zenye ubora na kisha kuongeza tija ya uzalishaji kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya Chakula na mahitaji ya Chakula na malighafi za Viwanda nchini na Nje.
Amesema kuwa katika kusheherekea siku ya Mbolea Duniani,Mamlaka imetolewa Mafunzo kwa wakaguzi wa Mbolea 169 kuwatambua na kuongeza Usajili wa wafanyabiashara kutoka 632 hadi 4,378 kuwafuatilia na kuwapa elimu ya utunzaji Bora wa Mbolea.
‘Kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 serikali ilitenga Fedha kiasi cha Shilingi Bill 150 kwa ajili ya kuanzisha mpango wa kutoa ruzuku kwenye Mbolea zote za kupandia na kukuzia’amesema Happiness
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema pia mafanikio mengine katika tasnia ya mbolea ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya viwanda vya kuzalisha mbolea nchini ambapo kabla ya mwaka 2016 vilikuwa vinne na hivyo kwa sasa kuna viwanda kumi na nane ambavyo huzalisha aina mbalimbali za mbolea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ruzuku kutoka TFRA Louis Kasera amesema kuwa mwaka huu wataendelea kutoa ruzuku kwa kuwasajili wakulima wapya huku malengo yakiwa ni kuwasajili wakulima Mill 7 mpaka kwaka 2025.
‘Katika mikoa ambayo inongoza kwa usajili ni Lindi ana watu Laki tatu na sabini na moja kisha Ruvuma ni laki tatu na arobaini na tatu na kumi na moja na mkoa wa mwisho ni Dar es salaam kuna watu elfu tano mia nne na sabini nahii ni kutokana na Jiografia hatulimi’amesema Kasera
Hata hivyo serikali imeendelea kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya kuzalisha mbolea hapa nchini ili kuendelea kukuza sekta hiyo.