Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeendesha warsha ya Machapisho ya Kisayansi (Scientific Journal) kwa wakurugenzi wa Utafiti na Machapisho kutoka Taasisi za Vyuo Vya Elimu ya Juu (HLI), tarehe 2 Oktoba 2023 ikilenga kuongeza tija na kuandaa Muongozo wa Kitaifa wa Utambuzi na Uhamasishaji wa Machapisho ya Kisayansi ‘National Guidelines for Recognition and Promotional of Scientific Journal in Tanzania’ ili kuendeleza utamaduni rasmi wa machapisho ya kisayansi yanayokidhi viwango vya ndani na Kimataifa. Warsha hiyo imefanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) tarehe 2 Oktoba 2023, Morogoro – Mjini.
Akifungua warsha hiyo, Kaimu Meneja wa Machapisho na Hifadhi Hati (DPU), Dkt. Wilbert Manyilizu alisema ili kuhakikisha Tume inawezesha huduma ya upatikanaji wa machapisho ya kwa umma kitaifa and kimataifa, na kuendeleza matumizi ya matokeo ya tafiti kwa kukuza sayansi na teknolojia kunahitaji chombo maalumu cha machapisho yanayoaminika na kukubalika Kimataifa na kuondosha changamoto ya mifumo kutosomana kwa kila Taasisi kusambaza matokeo ya utafiti kwa mifumo yake.
Mwezeshaji wa warsha hiyo kutoka Taasisi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Prof. Alexander B. Makullo alieleza kuwa lengo ni kupata muongozo wa Kitaifa utusaidie kuhamasisha matumizi ya machapisho ya kisayansi na kuondokana na dhana ya kulimbikiza jornal nyingi ambazo hazina muongozo wa pamoja.
“ Ni mumhimu kupata machapisho yanayotambulika Kimataifa na yanayoaminika , kwakuwa katika mawanda ya Kitaifa hayatambuliki rasmi , hivyo Tunaishukuru sana COSTECH kwa kuwezesha huu mchakato ni muhimu kupata muongoozo wa Kitaifa”
Warsha hiyo ilihudhuriwa na Wakurugenzi wa Tafiti na Machapisho toka Vyuo Vikuu ikiwemo Taasisi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Chuo Kikuu Huria (OUT), Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) pamoja na Chuo Kikuu cha Tina cha Kikristo Kilimanjaro (KCMUTCo).
Akihitimisha warsha hiyo Prof. Makullo, alifafanua kuwa COSTECH kupitia Sheria na. 7 ya mwaka 1986 Sehemu ya II, kifungu cha 5 (2), Kipengele (c) kinachipatia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ‘COSTECH’ jukumu la kukusanya, kuchakata, kuhifadhi na kusambaza Taarifa za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, hivyo mfumo huu utasimamia jukumu la mapitio na ithibati ya ubora wa machapisho ya majarida ya kisayansi.
Vilevile ni muhimu kwa Taifa kupata Mfumo wa Kitaifa kufanya upembuzi yakinifu wa viwango na ubora wa majarida ya kisayansi, kama inavyoelekezwa na muongozo ya Taasisi waambata wa COSTECH ikiwemo Tume Vyuo Vikuu (TCU) mwaka 2019 na Tangazo lake la Januari 2020 likiwalazimun walimu na wanafunzi wote kufanya machapisho pamoja na Bodi ya Huduma ya Maktaba Tanzania (TSLB), ambayo ina jukumu la kutoa rasilimali muhimu za ubora wa machapisho.