Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Cyriacus Binamungu akifundisha wanafunzi wa shahada ya uzamili kutoka vyuo mbalimbali nchini kuhusu kuandika makala ya kitaaluma yenye hadhi ya kuchapishwa na majarida, mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika katika Ndaki Chuo hicho kilichopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Masomo ya Utawala Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Mrisho Malipula akifundisha wanafunzi wa shahada ya uzamili kutoka vyuo mbalimbali nchini kuhusu kuandika makala ya kitaaluma yenye hadhi ya kuchapishwa na majarida, mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika katika Ndaki ya Chuo hicho kilichopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Bi. Membwana Ahmed akifundisha wanafunzi wa shahada ya uzamili kutoka vyuo mbalimbali nchini kuhusu kuandika makala ya kitaaluma yenye hadhi ya kuchapishwa na majarida, mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika katika Ndaki ya Chuo hicho kilichopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Marialauda Goyayi akifundisha wanafunzi wa shahada ya uzamili kutoka vyuo mbalimbali nchini kuhusu kuandika makala ya kitaaluma yenye hadhi ya kuchapishwa na majarida, mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika katika Ndaki ya Chuo hicho kilichopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Tafiti, Machapisho na Ushauri wa kitaaluma,Dkt. Darlene Mutalemwa akiwa na Mhadhiri Msaidizi Bi. Membwana Ahmed wakifatilia mada zinazowasilishwa wakati Mafunzo ya uandishi wa Makala za Kitaaluma, yaliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.
Washiriki wa mafunzo ya uandishi wa Makala za Kitaaluma wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi mafunzo hayo yaliyofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Dar Salaam
Wanafunzi wa shahada ya uzamili kutoka vyuo mbalimbali nchini wakiwa darasani katika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakijengewa uwezo kuhusu kuandika makala ya kitaaluma yenye hadhi ya kuchapishwa na majarida.
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuandika na kuchapisha makala za kitaaluma kwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamili.
Akizungumza katika mafunzo hayo leo Septemba 30, 2023 Jijini Dar es Salaam Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Cyriacus Binamungu, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali kutimiza matakwa ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ya kila mwanafunzi wa shahada ya uzamili ya kuandika makala ya kitaaluma yenye hadhi ya kuchapishwa na majarida yenye hadhi ya kitaaluma.
“Tunafundisha namna ya kuchagua mada, kuandika makala za kitaaluma kuanzia utangulizi hadi kufanya hitimisho pamoja na kuangalia mchango wa utafiti katika sera” amesema Prof. Binamungu.
Prof. Binamungu amesema kuwa kupitia mafunzo hayo wanaamini yanakwenda kuwasaidia wanafunzi kumudu takwa la kisheria la TCU.
“Mwanafunzi wanamawazo mazuri kuhusu makala wanayotaka kuandika, lakini hawana ujuzi au ufundi wa kuwasilisha kile wanachokijua katika mfumo ambao unatakiwa” amesema Prof. Binamungu.
Ameeleza kuwa uandishi wa makala za kitaaluma zina utaratibu wake “Baadhi ya wanafunzi hawajui kutengeneza mada inayotokana na tafiti walizofanya, pamoja na kuandika utangulizi ili kuwa na muunganiko mzuri kutoka sehemu moja kwenda nyengine”
Prof. Binamungu amefafanua kuwa washiriki wa mafunzo hayo watafundishwa na wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, huku akieleza kuwa ni mafunzo ya siku moja ambayo yatakuwa endelevu.
“Nawakaribisha wote ambao bado wanapenda kujifunza na kujipima ili kuongeza uwelewa, haya ni mafunzo endelevu yatakuwa yanatolewa kila mwezi ” amesema Prof. Binamungu.