Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati,Dkt Doto Mashaka Biteko amesema tayari Mkoa wa Geita unamiradi miwili ya umeme ukiwemo wa REA awamu ya Tatu Mzunguko wa pili pamoja na mradi wa kupeleka umeme kwenye migodi ya wachimbaji wadogo ambayo itasaidia kurahisisha kazi za wachimbaji na kukuza uchumi wa wananchi.
Biteko ameyasema hayo mapema leo wakati alipofika kwenye Kata ya Magenge na Kaseme Wilayani Geita kwaajili ya ziara ya kuwasha umeme na kukagua miundo mbinu ya umeme.
Amesema serikali inatambua Wilaya ya Geita inawachimbaji wengi wadogo na wanauwitaji wa umeme na wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwenye shughuoli zao kilio hicho serikali imekisia na mkakati ni kuweka umeme kwenye migodi yote ya wachimbaji wadogo.
“Tunayo migodi ambayo inatupatia uchumi mkubwa kwenye Wilaya ya Geita aina umeme kama ya Nyamalimbe na maeneo mengine naomba kuwaambia kuwa tunaleta umeme kwenye migodi yote ya wachimbaji wadogo Mama Samia Rais wetu amesikia kilio chenu wachimbaji na shughuli zimeshaanza za kuleta umeme kwenye Machimbo”Dkt Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
“Leo tupo hapa tumekuja kuwasha umeme tunataka tuwaone watanzania wavijijini wanautumia umeme kujiletea maendeleo,tunataka tuwe na nishati safi ya kupikia tunataka wakina mama waame kwenye matumizi ya kuni watumie nishati mbadala hii ndio nia ya Serikali ya awamu ya Sita”Doto Biteko Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati.
“Tuna fahamu watanzania wa vijijini wanaitaji pia mafuta waweze kufanya kazi zao na hakuna muwekezaji wa kuweka kituo cha mafuta tumekuja na mpango wa kuwakopesha wawekezaji waweke vituo kupitia mpango wa REA nia yetu ni kuhakikisha wananchi wa Kijijini wanaishi kama wapo Mjini”Dkt Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.