Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan amepongezwa kwa usimamizi mzuri wa sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu mipya ya elimu
Pongezi hizo zimetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Ilemela Wakili Mariam Abubakar Msengi wakati wa kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima nchini kwa mwaka 2023 kiwilaya yakifanyika katika viwanja vya Furahisha na kupambwa na kauli mbiu ya ‘Kukuza uwezo wa kusoma na kuandika kwa ulimwengu unaobadilika , kujenga msingi wa jamii endelevu na yenye amani’ ambapo amesema kuwa Rais Dkt Samia amekuwa msimamizi imara wa sekta ya elimu ya watu wazima na ujenzi wa miundombinu yake
“Tunampongeza Rais Dkt Samia kwa kuweka utaratibu mzuri katika sekta ya elimu, miundombinu inajengwa lakini pia walimu na mazingira ya kujifunzia yameboreshwa ‘” Amesema

Bi Msengi ameongeza kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kitengo cha elimu ya watu wazima kinazidi kuimarika na kwamba ni wajibu wa kila mmoja kuhamasisha watu kijunga na elimu ya watu wazima
Nae Tyson Charles kutoka taasisi ya elimu ya watu wazima jijini Mwanza amesema kuwa taasisi yake imekuwa ikihusika na uandaaji wa wataalam wanaotoa mafunzo mbalimbali ikiwemo walimu wa kufundisha wanafunzi waliokosa elimu katika muda rafiki kwao kama MEMKWA, Ujasiriamali na stadi za maisha sanjari na kuishukuru manispaa ya Ilemela kwa ushirikiano inaoutoa kwa taasisi hiyo
Bi. Redempta Kibiti ni afisa elimu msingi kitengo cha elimu ya watu wazima manispaa ya Ilemela ambapo amesema kuwa manispaa yake imepokea mradi wa SEQUIP na kushirikiana na Taasisi ya elimu ya watu wazima wenye lengo la kusaidia wanafunzi wasichana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 21 walioacha shule kwa matatizo mbalimbali ikiwemo mimba ambapo madarasa saba yameanzishwa kwenye shule 7 za Nyamanoro, Kabuhoro, Buswelu, Lukobe, Sangabuye, Lumala na Mnarani sekondari