Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi, akizungumza katika Kikao na Ujumbe wa Rais wa Kenya uliowasili nchini kujadili masuala mbalimbali ya kujifunza na kupata uzoefu wa namna Taasisi za Dini zinavyofanya kazi na jinsi zinavyosimamiwa nchini. Kikao hicho kilifanyika jijini Dodoma, leo Septemba 9, 2023. Kushoto ni Kiongozi wa Ujumbe huo, Mchungaji Alphonce Kange, na wapili kulia ni Msajili wa Jumuiya wa Wizara hiyo nchini, Emmanuel Kihampa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi, akizungumza katika Kikao na Ujumbe wa Rais wa Kenya uliowasili nchini kujadili masuala mbalimbali ya kujifunza na kupata uzoefu wa namna Taasisi za Dini zinavyofanya kazi na jinsi zinavyosimamiwa nchini. Kikao hicho kilifanyika jijini Dodoma, leo Septemba 9, 2023. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi (katikati meza kuu), akimsikiliza Msajili wa Jumuiya wa Wizara hiyo, Emmanuel Kihampa alipokuwa akiwasilisha taarifa yake kwa Ujumbe wa Rais wa Kenya, kuhusu Taasisi za Dini zinavyofanya kazi na jinsi zinavyosimamiwa nchini, katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma, leo Septemba 9, 2023. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi wa Ujumbe wa Rais wa Kenya, Sheikh Muhammad Dori akizungumza katika kikao kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ujumbe wa Rais wa Kenya, kilichofanyika jijini Dodoma, leo Septemba 29, 2023. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi, wapili kulia ni Kiongozi wa Ujumbe huo, Mchungaji Alphonce Kange na kushoto ni Msajili wa Jumuiya wa Wizara hiyo nchini, Emmanuel Kihampa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Msajili wa Jumuiya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Kihampa akizungumza na Ujumbe wa Rais wa Kenya baada ya kuwasilisha taarifa yake kuhusu Taasisi za Dini zinavyofanya kazi na jinsi zinavyosimamiwa nchini, katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma, leo Septemba 9, 2023. Kushoto ni Kiongozi wa Ujumbe huo, Mchungaji Alphonce Kange. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………………..
Na Mwandishi Wetu, MoHA, DODOMA.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi, ameongoza Kikao na Ujumbe wa Rais wa Kenya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, Mtumba jijini Dodoma, leo Septemba 29, 2023.
Ujumbe huo kutoka nchini Kenya, uliwasili Jijini Dodoma kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu wa namna Taasisi za Dini zinavyofanya kazi na jinsi zinavyosimamiwa nchini.
Kabla ya Msajili wa Jumuiya wa Wizara, Emmanuel Kihampa hajatoa taarifa yake kuhusu utendaji kazi wa Jumuiya hiyo, Dkt. Kazi aliwakaribisha wajumbe hao kutoa taarifa yao ya nini wanachohitaji kujua zaidi kuhusu Taasisi za dini zinavyofanya kazi nchini.
Kiongozi wa Ujumbe huo, Mchungaji Alphonce Kange, alisema Tanzania ni Jirani na Kenya, ni ndugu hivyo wapo nyumbani kwa kujifunza mambo mambo mazuri kutoka nchini hasa kuhusu kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wa Taasisi za Dini na jinsi zinavyosimamiwa Tanzania.
Kenya inafanya maboresho ya sheria zinazohusiana na usajili na usimamizi wa Taasisi za Dini nchini humo hivyo ziara yao Tanzania ni kuja kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na Taasisi za dini jinsi zinavyofanyakazi pamoja na kusimamiwa.