Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) akizungumza na wanachama wa cha cha wachimabaji madini wanawake Tanzania TAWOMA katika mkutano wa kijadiliana Changamoto na mafanikio ya ushiriki wa wanawake katika shughuli za uchimbaji madini ukiofanyika. Kwenye viwanja vya EPA Bombambili mjini Geita.
Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Dhahabu ya BUCKREEF Amelda Msuya akifurahia jambo na Afisa Mawasiliano wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO wakati wa mkutano wa TAWOMA uliofanyika kwenye ukumbi wa mkapa katika maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima, wa pili kutoka kulia akifuatilia mkutano huo kwa kuandika mambo muhimu yaliyoainishwa na wachimabaji madini wanawake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa GGR Sarah Masasi katika mkutano huo.
…………………………….
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) amesema shirika hilo linategemea kuwapa mafunzo wanachama wa chama cha wachimbaji madini nchini (TAWOMA) ili chama chao kiwe na nguvu kwa vijana wanawake kujiunga na chama hicho.
Haya ameyasema leo Septemba 29, 2023 wakati akizungumza na wanachama wa TAWOMA kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Mkapa Mkoani wakati wa maonyesho ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili.
Dkt. Mwase Amesema lengo la kuwaendeleza vijana wanawake (TAWOMA Youth) ni kuwafanya vijana wengi waweze kuingia kwenye shughuli za uchimbaji madini shughuli ambazo zitaongeza ajira na kuwainua kiuchumi.
“Tumekua tukifanya juhudi mbalimbali ili kuahakikisha tunalinda nguvu kazi tulifanya safari kwenda China na tulienda nao na tumewasaidia vijana na tumesaidia mashine ambazo watazitumia kwenye shughuli zao za kazi za madini”.
Amesema katika kuwaongezea shughuli za kiuchumi shirika limekuja na bidhaa ya nishati safi ya kupikia na kuwapa uwakala TAWOMA lengo ni kuwasaidia kuwa na njia nyingi za kujipatia kipato.
“Navutiwa ninaposapoti kitu na kinaenda vizuri inatia moyo mimi kama mlezi wenu na nitaendelea kuisaidia TAWOMA na kuhakikisha inafika mbali zaidi na kufikia malengo mliojiwekea kwa maslahi yenu na taifa kwa ujumla”amesema Mwase.
Aidha Mwase ameupongeza uongozi wa TAWOMA kwa kuwa na katiba nzuri inayosimamia shughuli zao za kila siku lakini pia kwa kuwa na bodi yenye kamati zote zinazosimamia shughuli zao lakini pia kuwa na mfumo mzuri wa kifedha.
Amesema kupitia tasnia ya madini nchini inaweza kuleta mageuzi katika kumuwezesha mwanamke kufikia malengo aliyojiwekea kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na nchi ili kufikia maendeleo endelevu SDG yaliyowekwa.
Serikalia inapaswa kuratibu shughuli zinazofanywa na wachimbaji wanawake ili kuwawezesha kiuchumi na kuiweka nchi katika nafasi nzuri katika sekta ya madini.