K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAAJIRI
kote nchini wamehimizwa kutumia TEHAMA kuwasilisha taarifa kuhusu mfanyakazi
aliyepata Ajali, Ugonjwa au Kifo kilichotokana na kazi aliyoajiriwa kwa mujibu
wa mkataba wa ajira yake, ili
kurahisisha mchakato wa malipo ya fidia.
Wito
huo umetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. John Mduma, wakati akifungua semina kwa maafisa rasilimali
na maafisa usalama na afya mahali pa kazi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema,
kwa majukumu waliyonayo maafisa hao kutoka kwenye kampuni wanazoziwakilisha, wao
ni kiungo muhimu kati ya mwajiri na WCF, na kwamba Mfuko, umehakikisha
unarahisisha utoaji wa huduma ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na kwa
sasa huduma zote zinapatikana mtandaoni kupitia (portal.wcf.go.tz).
“Uzoefu wetu unaonyesha
uptake ipo ya kutosha ya huduma zetu na hasa huduma zinapatikana mtandaoni, ni
rai yangu kuendelea kuwahimiza kutumia mitandao inayotoa huduma za WCF, na sit u kurahisisha utoaji huduma, lakini pia
kupunguza gharama na muda na hivyo kuharakisha utoaji wa malipo ya Mafao ya
fidia.” Alisisitiza.
Alisema
Mfuko upo kwa nia ya kuwaondolea watu watakaopata madhila yatokanayo na kazi,
madhara ya kijamii, kiuchumi na hasa kuchangia katika kuhakikisha kwamba kipato
cha wanaopatwa na madhara haya hakiyumbi kama ambavyo sera inavyoelekeza.
Aidha,
Dkt. Mduma alisema, serikali ilianzisha
Mfuko huo ili ubeba jukumu la kumuhudumia mfanyakazi aliyeumia au kuugua
kutokana na kazi, huku mwajiri yeye abaki
na jukumu la uzalishaji na kusimamia uendelevu wa biashara zake na hivyo
kuchangia ukuaji wa uchumi wanchi.
“Tunaamini kwa
kuyatenganisha haya tuko kwenye model nzuri ya hifadhi ya jamii kwenye eneo la
Fidia kwa Wafanyakazi kuliko ilivyokuwa hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa
Mfuko.” Alibainisha.
Akizungumzia
kuhusu yale yaliyofundishwa kwenye semina hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini
WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema washiriki wamejifunza namna ya kutoa
taarifa za ajali au magonjwa yatokanayo na kazi kwa njia ya mtandao ikiwemo kutuma
madai, lakini pi walijifunza kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi
ikiwemo jinsi ya kubaini vihatarishi maeneo ya kazi.
Kwa
upande wao, washiriki wameipongeza WCF kwa utaratibu huo wa kuendelea kutoa
elimu kwa makundi mbalimbali kuhusu elimu ya fidia kwa wafanyakazi.
Bi.
Zainab Jereko, ambaye ni mshiriki, aliwaasa waajiri kuzingatia usalama na afya mahali pa
kazi, ambapo alisema inagawa WCF ipo kwa ajili ya kutoa fidia, lakini hiyo
haiondoi wajibu wa waajiri kuzingatia usalama na afya mahali pa kazi unakuwepo.
Bi. Jereko pia alisifu mfumo wa kufungua madai kupitia mtandao, “umekuwa na msaada
mkubwa kwa waajiri kwani umerahisisha utoaji taarifa lakini pia umeondoa
usumbufu na upotevu wa muda wa kwenda
ofisi za WCF ili kutoa taarifa.” Alisema Bi. Jereko.
“Pamoja
na yote niliyojifuzna nimefurahia sana namna Mfuko ulivyoweka mifumo ya kisasa
ya utoaji taarifa kwa njia ya mtandao endapo itatokea ajali eneo la kazi.” Alisema
mshiriki mwingine Bw.Goodlove Bugenyi.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, mwajiri yoyote Tanzania Bara
anawajibika kujisajili katika Mfuko.
Mwajiri
anaweza kujisajili katika Mfuko kwa njia ya mtandao (portal.wcf.go.tz) au
kwakujaza Fomu za usajili (WCR-1 na WCR-2) na kuziwasilisha kwenye ofisi ya
Mfuko iliyopo karibu nae au ofisi za idara ya kazi.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar
Meneja Tathmini Vihatarishi mahali pa Kazi, Bi. Naanjela Msangi, akitoa ‘darasa’ kuhusu hatua mbalimbali za kuchukua ili kubaini vihartarishi vinavyoweza kupelekea ajali au magonjwa mahali pa kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidida kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. John Mduma (kushoto) akimkabidhi kitendea kazi, Bi. Secillia Assey, huku Meneja Tathmini Vihatarishi mahali pa Kazi, Bi. Naanjela Msangi, akishuhudia.