…………………
Na. Sixmund Bagashe – Arusha
Jeshi la Uhifadhi nchini limepewa kanuni nane zitakazo wezesha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya Uhifadhi wa raslimali zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Akizungumza Jijini Arusha na Maafisa wa Taasisi nne zinazounda Jeshi hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Dkt. Hassan Abbas amezitaja kanuni hizo kuwa ni pamoja na malengo, kasi ya kufikia malengo, kutekeleza malengo, ushirikiano kazini, matumizi sahii ya muda, maadili, mawasiliano pamoja na ucha Mungu.
Sambamba na hayo, Dkt. Abbas ameongeza kuwa ili waweze kutimiza malengo yaliyopo kupitia kanuni hizo nane Mhifadhi wa Jeshi hilo hana budi kuwa na maadaili yatakoyomsaidia kufikia ma lengo hayo.
Dkt. Abbas amewataka Maaskari wa Jeshi hilo kuhakikisha wanazingatia kikamilifu suala la maadili kazini na kuwa uongozi wa Wizara hiyo hautosita kuwachulia hatua kali wale wote watakao kwamisha malengo ya Jeshi hilo kwa kuwa na maadili mabaya.
Vilevile, Dkt. Abbas amezisisitiza Taasisi hizo kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozifanya za kutangaza Utalii kupitia Filamu ya The Royal Tour Kwa kuhakikisha suala la Mawasiliano linapewa kipaumbele hasa katika kutoa taarifa kwa umma juu ya matokeo chanya ya utekelezaji wa kazi zao na kutangaza kwa nguvu zote vivutio vilivyo chini yao.
Awali akimkaribisha Katibu Mkuu Dkt. Abbas, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba ameeleza kuwa warsha hiyo kwa Maafisa wa Jeshi la Uhifadhi imelenga kukumbushana masuala mbalimbali ya uhifadhi pamoja na haki za binadamu.