Msajili wa Baraza la Famasi nchini, Elizabeth Shekalaghe amesema Baraza hilo linashiriki katika mkutano wa mawaziri wa afya na UKIMWI wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya SADC kuona ni mambo gani yatakayojadiliwa katika mkutano huo ili na kuona namna nzuri ya kuibua hoja ya wataalamu wa mabaraza ya afya katika nchi hizo watakavyoweza kushiriki katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo. Aidha, alipendekeza kuwepo kwa ushirikiano na kubadilishana utaalamu hapo baadaye ya namba ya uboreshaji wa huduma zinatotolewa kwa wagonjwa.
Bi. Elizabeth Shekalaghe ameyasema hayo katika banda la baraza hilo kwenye maonesho yanayoendelea kando ya mkutano wa mawaziri wa Afya na UKIMWI wa nchi za SADC unaofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Amesema kwa upande wa Mabaraza ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kumekuwa na ushirikiano mkubwa kwa wataalam wa taaluma ya famasia wa nchi hizi ili kuhakikisha mifumo ya usimamizi wa dawa kwa watumiaji.
“Kama wataalamu wa afya ikiwepo famasi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mabaraza yamekuwa yakikutana na kufanya vikao mbalimbali ili kujadili changamoto zinazowakabili wakiwepo wataalamu wa famasia na kuona ni namna gani tunaweza kupiga hatua katika utaalamu wa huduma hiii muhimu katika afya”. Amesema Bi. Elizabeth Shekalaghe
Ameongeza kuwa kama itawezekana suala la ushirikiano katika nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za SADC pia hapo baadae linaweza kufanyika na itakuwa ni hatua muhimu sana kufikiwa kwani itaweza kuongeza wigo wa kubadilishana uzoefu na utaalam wa shughuli za wafamasia katika mabaraza ya nchi za ukanda huo.
Hapa nchini bado idadi ya wataalamu katika fani ya famasi sio ya kuridhisha pamoja na umuhimu wa kuwepo usimamizi wa karibu wa fuduma hizi. Takwimu zinaonesha kuwamwaka 2013 kulikuwa na wafamasia 1245 na kufikia sasa kuna wafamasia 18670 jambo ambalo linaonesha umuhimu wa kuwepo kwa wataalamu wa famasi na wanatakiwa kuongezeka zaidi ili kuboresha mazingira ya huduma hii.