Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mhe.
Constantine John Kanyasu ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA kwa kushiriki Maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini 2023.
Mhe. Kanyasu ametoa pongezi hizo tarehe 26 Septemba,2023 alipotembelea Banda la TPA katika maonesho hayo yanayoendelea Katika Viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita.
Aidha Mhe. Kanyasu ameshauri Elimu zaidi iendelee kutolewa kwa Umma kuhusu huduma zinazotolewa na Bandari kutoa Rai kwa Wakazi wa Geita na Wananchi wanaofika Katika Maonesho hayo, kutembelea Banda la TPA ili kujifunza mengi kuhusu Shughuli za Kibandari
Katika picha akipata maelezo kutoka kwa Deniss Mapunda wakati Afisa Utekelezaji TPA wakati alipotembelea katika banda hilo.
Katika picha akipata maelezo kutoka kwa Deniss Mapunda wakati Afisa Utekelezaji TPA wakati alipotembelea katika banda hilo.
Katika picha akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea katika banda la TPA kwenye maonesho ya Madini kwenye viwanja vya Bombambili mjini.
Katika picha akipokea zawadi kutoka kwa Deniss Mapunda Afisa Utekelezaji TPA alipotembelea wakati alipotembelea katika banda la TPA kwenye maonesho ya Madini kwenye viwanja vya Bombambili mjini.