Sophia Kingimali
Shirika la Maendeleo ya Taifa NDC limesema pamoja na mafanikio wakiliyoyapata kwa kipindi cha mwaka mmoja wamejipanga kuendeleza rasilimali za kimkakati za nchi kwa kuzingatia mazingira ya sasa.
Akizungumza Leo septemba 26 jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji na vipaumbele vya shirika kwa mwaka 2023/2024 Mkurugenzi Mwendeshaji wa ShirikaDkt Nicolaus Shombe amesema muundo wa shirika utaangaliwa upya kwa ajili ya maslahi ya kibiashara ili kusimamia mwelekeo kiuchumi wa nchi
“Tutambue ya kuwa nchi zote duniani zina mashirika au taasisi ambazo zinaangalia maslahi ya kibiashara ya nchi hizo hivyo na sisi tumejipanga vizuri kwenye hilo”
Akielezea mafanikia ya shirika amesema mafanikio mengi yaliyopatikana yametokana na juhudi za serikali kwa kujenga uchumi imara usio tegemezi.
Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja shirika limefanikiwa kutekeleza mradi wa kimakakati wa Ligaga na Mchuchuma wenye thamani ya Trillioni 8.
Amesema utekelezaji wa mradi huo umepanga kuchimba chuma Tani milioni 2.9 kwa mwaka na kuzalisha bidhaa za chuma Tani milioni 1 kwa mwaka.
Amesema mradi wa Liganga na Mchuchuma ni tofauti na miradi mingine kwani ni mradi wa kimkakati na kielelezo kilichobainishwa katika dira ya maendeleo ya Taifa 2025.
“Shirika limefanikiwa kulipa fidia kwa jumla ya shilingi15,424,364,900 kwa wananchi wanaopisha utekelezaji wa miradi ambapo Mchuchuma shilingi bilioni4 na Liganga bilioni 10 thamani ya mradi.” Amesema Shombe.
Amesema kufuatia mageuzi na mabadiliko yaliyofanywa na shirika NDC linasimamia miradi 8 ya viwanda mama inayojumuisha miradi mitatu ya makaa ya mawe ya Mchuchuma,Kate Katewaka na Ngaka.
Aidha Chombe ameongeza kuwa katika kusimamia kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo zao la mpira serikali imepanga kupanda miche mipya 20,300 ya mpira katika eneo la hekta 45 katika Shamba la mpira la Kalunga na Kihuhwi.
Shirika limekua likisimamia na kutekeleza miradi ya kiuchumi ambayo inagusa sekta muhimu za kilimo,viwanda,madini,nishati miundombinu ya kibiashara lengo likiwa kuharakisha maendeleo endelevu nchini ambapo mpaka sasa limetekeleza miradi mbalimbali nchini ambayo imeleta tija kwa taifa.