Wakizungumza na wafuasi wao mbele ya madhabahu ,viongozi wa madhehebu mbalimbali akiwemo Mchungaji Nelson Godiwe,Padre Fransisco Chengula na Ostadhi Hamis Johari wamesema suala la kolipa kodi ni takwa la kimungu kwasababu hata maandiko matakatifu yameagiza hivyo kila mteja ana jukumu la kudai risiti na muuzaji kutoa risiti ili kuchangia pato la taifa
Awali wakati akizinduzi wa kampeni ya “Tuwajibike ” kimkoa, Meneja wa TRA mkoa wa Njombe Spesioza Owure amesema mkoa wa SW umepangiwa kukusanya bil 17 hivyo kila myanya ya upotevu wa mapato inapaswa kuzibwa ili kuokoa mapato yanayovuja
Meneja Owure amesema uzinduzi wwa kampeni hiyo ya awamu ya pili unakwenda kujikita zaidi katika kuhamasisha kutoa risiri na kudai risiti katika mauziano na kisha kudai kwamba elimu inakwenda kuongezwa kwa jamii ili kupata fedha za ushuru kwa maendeleo ya taifa .
Kwa upande wao wanafunzi akiwemo Innocent Paul wanasema elimu waliyopatiwa inakwenda kutekelezwa kwa vitendo kwa kudai risiti manunuzi ya mahitaji yote ya shule kwasababu kupitia kodi za watanzania serikali inatoa elimu bure