Na Sophia Kingimali
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS kimezindua kitabu cha afya,usalama mahara pa kazi na tiba lengo likiwauh kuelewesha watoa huduma na wagonjwa madhara yatokanayo na kazi na uwezekano wa fidia pindi wafanyakazi pindi wanapopata matatizo wawapo kazini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hiko Leo septemba 25 jijini Dar es salaam kaimu naibu mkuu wa chuo MUHAS Prof.Emmanuel Balandyo amesema kitabu hiko kitatumika katika vyuo ili kusaidia kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kulinda afya zao pindi watakapokuwa kazini.
“MUHAS tumeshirikiana na OSHA na WCF kuandaa kitabu hiki lengo ni kuhakikisha elimu ya usalama mahala pa kazi inawafikia watu wote ili kuepuka majanga”amesema Balandyo
Amesema pamoja na kitabu kufundishia wanafunzi lakini pia kitatumika kutoa maelekezo kwa wafanyakazi namna ya kujikinga na dhidi ya majanga wawapo kazini.
Kwa upande wake mkaguzi wa afya OSHA Amina Nangu amesema kitabu kitatoa uelewa kwa wafanyakazi kuhusu kulinda afya zao kwa kuepuka majanga pindi wa wapo kazini.
“Sasa hivi afya mahala pa kazi si sheria tu Bali ni haki ya msingi kwa kila binadamu”amesema Nangu
Nae,Meneja wa WCF Naanjela Msangi amesema usalama na afya mahala pa kazi vikilindwa vitasaidia mfuko kutoelemewa lakini nchi kufikia kwenye maendeleo endelevu kama ilivyojiwekea.
Sambamba na hayo Muhariri wa kitabu hiko Dkt Israel Nyarubeli amesema dhima kubwa la kitabu hiko ni kutambua magonjwa na ajali ambazo zinaweza kujitikeza mahali pa kazi.
Amesema wafanyakazi wanapaswa kutambua viatarishi pindi wawapo kazini ili kujikinga.
“Kitabu hiki kinasura 8 ambapo kimeandikwa na waandishi 13 kutoka taasisi sita hivyo kitabu hiki pamoja na kutumika kama maelekezo kwa wafanyakazi lakini pia kitatumika kuwafundishia wanafunzi ili waweze kujiandaa wanapoenda kazini”amesema Nyarubeli