Naibu Waziri MKuu na Waziri wa Nishati Mhe Dkt Doto Biteko amefurahishwa na jinsi STAMICO invyoendelea kuwasaida wachimbaji wadogo.
Hayo amesema leo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya kiteknolojia ya Madini wakati alipotembelea banda la STAMICO yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili Mkoani Geita kuanzia tarehe 20 hadi 30 Mwenzi Septemba 2023.
Awali akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwase amesema wataendelea kuwawezesha watu wa makundi maalum ili waweze kujikimu kimaisha.
Amesema STAMICO wamekuwa wakifanya ubunifu mbalimbali kwa ajili ya watu wa makundi maalumu ambapo kati ya bunifu hizo wameweza kubuni mkaa mbadala ambao umekuwa fursa kwa vikundi mbalimbali.
“Tumeleta nishati mbadala kwa ajili ya kupikia ili kutunza mazingira na kupunguza ukataji wa miti ambao unaathiri mazingira”
Amesema bidhaa hiyo inapaswa itumike na makundi maalum kama fursa ya kujiongezea kipato
“Tumekua tukifanyakazi kwa karibu na watu wa makundi maalumu Dodoma tumeshakaa na ndugu zetu walemavu wa ngozi, lakini pia kuna makundi yenye usikivu hafifu vilevile tumeweza kuwawezesha vifaa na elimu nao sasa hivi wanafanya vizuri kwenye madini. Aidha kuna kikundi cha wanawake na Samia wa hapa Geita nao tumewapa uwakala wa nishati mbadala amesema Dkt Mwasse
Ameongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha uchumi wa taifa unakua lakini kila mtu anajipambanua katika ukuaji wa uchumi huo.
Kikundi cha Wanawake na Samia cha Mkoani Geita ambacho kinafadhikiwa na STAMICO na ni mawakala wa mkaa mbadala Mkoani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwase akijadiliana jambo na wana kikundi cha walemavu wa ngozi kutokea Mkoani Dodoma ambacho pia ni mawakala wa mkaa mbadala Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwase akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimnaji wadogo Wanawake ambao ni wanachama wa TAWOMA.