MKurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini STAMICO Dkt. Venance Mwase akizungumza na Meneja Masoko na Mawasiliano wa STAMICO Bw. Geofrey Meena katika maonesho ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita ambapo STAMICO inashiriki katika maonesho hayo.
MKurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini STAMICO Dkt. Venance Mwase akizungumza navijana wenye ulemavu wa ngozi kutoka mkoani Dodoma ambao wanadhaminiwa na STAMICO na ni mawakali wa kuuza mkaa mbadala kutoka mkoani Dodoma wakishiriki kwenye maonesho ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita ambapo STAMICO inashiriki katika maonesho hayo.
MKurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini STAMICO Dkt. Venance Mwase Meneja Masoko na Mawasiliano wa STAMICO Bw. Geofrey Meena wakiwa wamekaa pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo katika maonesho ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita ambapo STAMICO inashiriki katika maonesho hayo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa STAMICO Bw. Geofrey Meena akizungumza na akina mama wa Kikundi cha Wanawake na Samia Mkoani Geita katika maonesho ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mjini Geita ambapo STAMICO inashiriki, Kikundi cha Wanawake na Samia Geita pia kinadhaminiwa na STAMICO na ni mawakala wa kuuza mkaa mbadala mkoani humo.
Akina mama wa kikundi cha Wanawake na Samia Geita kikiwa katika picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake na Samia Geita Bi. Adelina Kabakama akizungumzia ushiriki wao katika maonesho ya madini yanayofanyika mjini Geita.
………………………………..
Wanawake wa Kikundi cha Wanawake na Samia cha Mkoani Geita wamelishukuru Shirika la Madini la Taifa STAMICO kwa kuwawezesha wanawake katika Shughuli za kiuchumi ili kuinua kipato.
Akizungumza Leo Septemba 23, 2023 kwenye maonyesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita mwenyekiti wa kikundi hiko Adelina Kabakana amesema STAMICO wamewezesha zoezi la kupanda miti mkoani Geita ambayo wanaendelea kuitunza kwa maslahi ya nchi.
“Tunajua kwamba mazingira yakiharibika mwanamke ndio anaoathirika kwanza “amesema Kabakama.
Sambamba na haya Bi Kabakana amesema STAMICO imewasaidia katika harakati za kupinga ukatili wa kujinsia kwa kuwatafutia shughuli za kuwapatia kipato na kuwatoa kwenye utegemezi hali iliyokua inapelekea wanawawake hao kuingia kwenye ukatili.
Amesema STAMICO wamewawezesha kuwatafutia soko la mkaa mbadala wanaouzalisha ambapo mkaa huo umekua suluhisho la ukataji wa miti na utunzaji wa mazingira lakini pia kupunguza ukatili wa kijinsia kwa kukuza uchumi wa familia.
“Uwakala huu umesaidia kurudisha furaha kwenye Familia na kuondoa ukatili kwani vipato vya familia vimeongezeka , Unajua mama akiwa na uchumi wake na baba akiwa na uchumi mzuri ukatili hautokuwepo kwenye Familia hivyo tunaungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hasan katika jitihada zake za kuwasaidia wanawake vijana na watu wenye makundi maalumu”amesema Kabakama.
.……………………….
Kikundi cha Wanawake na Samia cha Mkoani Geita wamelishukuru Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuwawezesha wanawake katika Shughuli za kiuchumi ili kuinua kipato.
Akizungumza Leo Septemba 23, 2023 kwenye maonyesho ya madini yanayofanyika kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita mwenyekiti wa kikundi hicho. Bi Adelina Kabakana amesema STAMICO wamewezesha zoezi la kupanda miti Mkoani Geita ambayo wanaendelea kuitunza kwa maslahi ya nchi.
“Tunajua kwamba mazingira yakiharibika mwanamke ndio anaoathirika kwanza “amesema Kabakama.
Sambamba na haya Bi Kabakana amesema STAMICO imewasaidia katika harakati za kupinga ukatili wa kujinsia kwa kuwatafutia shughuli za kuwapatia kipato na kuwatoa kwenye utegemezi hali iliyokua inapelekea wanawawake hao kuingia kwenye ukatili.
Amesema STAMICO wamewawezesha kuwapa Wakala wa Nishati Mbadala kwa Mkoa wa Geita.
Nishati hiyo ni suluhisho la ukataji wa miti hovyo na itasaidia sana utunzaji wa mazingira lakini pia kupunguza ukatili wa kijinsia kwa kukuza uchumi wa familia.
“Uwakala huu umesaidia kurudisha furaha kwenye Familia na kusadia kuondoa kuni kichwani kwa kina Mama na kuondoa ukatili kwani vipato vya familia vimeongezeka.
Unajua mama akiwa na uchumi wake na baba akiwa na uchumi mzuri ukatili hautokuwepo kwenye Familia hivyo tunaungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hasan katika jitihada zake za kuwasaidia wanawake vijana na watu wenye makundi maalumu”amesema Kabakama.
Meneja Masoko wa STAMICO Bw. Geofrey Meena akizungumza kwa upande wa Stamico alisema Stamico itakuwa tayari kufanya kazi na kikundi hiki ili kiweze kufikia malengo waliyojiweke kwa kuwapatia bidhaa bora na safi na salama ya kupikia – Rafiki Briquttes