………………………….
Na Sophia Kingimali
Na Sophia Kingimali
Katika kuendelea kuboresha mifumo ya Tehama nchini serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) umetangaza rasmi kuufunga mfumo TANeps ifikako septemba 30 hivyo ametoa rai kwa taasisi zote za umma kujiunga kwenye mfumo mpya wa manunuzi wa kielekroniki wa Taifa ufahamikao kama e-Procurement System of Tanzania (NeST) na kulazimika kuachana na ule wa awali ambao hakuwa salama kwa usalama wa nchi.
Hayo ameeleza septemba 22 Afisa mtendaji mkuu wa PPRA Eliakim Maswi jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya habari nchini, amesema kuwa baada ya Serikali kufanya tathmini ya kina ya mfumo uliopo wa TANePS wataalamu walishauri kujengwa kwa mfumo mpya ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto kwani mfumo ulipo sasa haukidhi mahitaji ya Serikali.
Amesema Mfumo wa NeST utakuwa na uwezo wa kuongeza uwazi na uwajibikaji na utakidhi mahitaji ya sheria za nchi, taratibu na miongozi ya ununuzi. Lakini pia kuwa na mfumo wa NeST unakwenda kupunguza mianya ya rushwa na kuleta thamani halisi ya fedha za Serikali katika ununuzi wa umma.
“Lakini pia utakuwa mfumoutakaokuwa rahisi katika kutumia na kuongeza wigo kwa watumiaji. Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Serikali Mtandao (eGA) iliamua kufanya tathmini, ambapo Februari 2022 ilionekana wazi kwamba mfumouliopo hauwezi kukidhi mahitaji ya sasa ya Serikali ni vigumu kuweza kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na uendeshaji wa mfumo, ambapo sasa hata sisi PPRA tukitaka jambo lazima tuwasiliane na mwendeshaji ambaye yupo Ugiriki.amesema
Aidha ameongeza kuwa timu ya wataalamu iliishauri Serikali ianze kazi ya kujenga mfumo mpya pamoja na kutatua changamoto zilizopo kwenye mfumo uliopo.
Amesema Serikali ilipomtaka mzabuni aweze kuwezesha Serikali kuwa na Full control ikiwemo kuwa na Full Source Code, mzabuni aliiambia Serikali italazimika kulipa Dola za Marekani milioni 25 (zaidi ya Shilingi bilioni 65),” amesema Maswi
Kutokana na hali hiyo Maswi, amesema kuwa iwapo Serikali ingelea kurithi matatizo yaliyopo kwa sasa ya kuwa na mfumo ambao haukidhi mahitaji ya watumiaji na kama itataka mfumo huo uhuishwe, Serikali italipa gharama kubwa.
“Uwezekano wa gharama za kuhudumia kuwa kubwa kutokana na mkandarasi kutokuwa na ushindani. Iwapo Serikali itaamua iisingie mkataba mpya na mkandarasi na kuamua kutumia mfumo ulivyo, changamoto itakuwa kubwa wakati wa matumizi kwani wataalamu wa Tanzania hawana ujuzi wa kuhudumia mfumo”amesema
Aidha Maswi, amesema kuwa changamoto nyingineni mkataba wa mkandasi wa kuhudumia mfumo unaisha Desemba 31,2023 na iwapo Serikali isingeweza kuwa na mfumo mbadala wakati huu yapo masuala kadhaa yangejitokeza ikiwamo muda wa vifaa utakuwa umemalizika na Kampuni ya European Dynamics ingeitaka Serikali inunue vifaa vingine kulingana na matakwa yao wenyewe na sio mahitaji ya Serikali.
Maswi, amesema kuwa hadi kufikia Juni 2023 taasisi nunuzi 864 zimesajiliwa kwenye mfumo na ndio zilizopaswa kutumia mfumo huoambapo wazabuni 37, 445 wamesajiliwa kwa ajili ya kutumia mfumo.
Amesema tangu kuanza kutumia mfumo zaibuni 142,606 zilitangazwa kwa kutumia mfumo wa zabuni zilizoendela hadi kupata tuzo kwa kutumia mfumo ni 26,366 sawa na asilimia 18.5 na hivyo kuonesha kiwango kidogo katika kukamilisha mchakato wa ununuzi kwa kutumia mfumo huo.
Kati ya zabuni zilizotangazwa zaidi ya asilimia 81.5 ya zabuni hizo hazikumaliza mchakato wake kwa kutumia mfumo. Wakati mfumo wa sasa wa NeST ni rahisi na unatumia dakika 30 na umeunganishwa na taasisi zote ikiwemo Brela taasisi hivyo PPRA ataweza kuona kila kitu kwa wakati huohuo jambo ambalo litaleta ushindani wa kweli na wa haki.
“Tunajua wapo waliokuwa wakiomba zabuni maana halisi ya zabuni kuomba mtandaoni ni kupunguza na kuondoa kabisa rushwa lakini kupitia mfumo huu mpya mengi tunayaona kwa wakati na hata kuweza kuwasiliana na wahusika kama kuna jambo ambalo haliko sawa,” amesema Maswi.
Amesema mfumo wa NeST utasaidia kudhibiti rushwa, mchakato wa zabuni kuchelewa na kuongeza uwazi wa zabuni.
Mfumo huo uliobuniwa na kutengenezwa na watanzania wenyewe umeanza kufanya kazi Julai 1, mwaka huu ukichukua nafasi ya mfumo wa awali wa TANePS utakaokoma kufanya kazi itakapofika Septemba 30, mwaka huu.
Maswi amewataka wafanyabiashara wote kuomba zabuni kwa kutumia mfumo huo mpya kama wanataka kupata kazi za serikali.
Amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kubadilisha utendaji wa mamlaka hiyo na anataka itoke mahali ilipo kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo matumizi ya mifumo ya kielektroniki kuleta tija na ufanisi unaostahili.
Amesema taasisi zinazosimiwa na Msajili wa Hazina na Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (TAMISEMI), zinapaswa kuanza kutumia mfumo mpya kwa shughuli za ununuzi wa umma na kwamba itakapofika Oktoba Mosi mwaka huu taasisi nunuzi zote za serikali hazitaweza kutuma mialiko ya zabuni katika mfumo wa zamani wa TANePS.