Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dr. Joseph Kimaro.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, kwa kushirikiana na Manispaa ya Wilaya ya Temeke,imeendesha Kambi ya Matibabu katika kituo cha afya cha Yombo Vituka,kwa lengo la kutoa huduma bora za afya za kibingwa na kibingwa bobezi kwa wakazi wa Temeke na maeneo jirani.
Kambi hiyo imehusisha madaktari bingwa na bingwa bobezi kutoka fani mbalimbali kama vile, kisukari, figo, moyo, mfumo wa mkojo, mishipa ya fahamu, watoto, afya ya akili, meno, mifupa, macho, lishe, mazoezi(Physiotherapy), wanawake na uzazi, masikio, pua na koo. Na kufanikiwa kutoa huduma ya kiuchunguzi na tiba kwa watu 636.
Wakati wa kuhitimisha kambi hiyo, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dr. Joseph Kimaro amesema kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke inaendelea kuunga mkono jithada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kusogeza huduma za ki bingwa na bingwa bobezi karibu na wananchi hivyo wakazi wa Temeke wanaweza kutegemea huduma bora za afya na kupitia Kambi hii ya Matibabu imewafikia watu 636. Na kuongeza kuwa ikiwezekana kambi hii iwe ndelevu ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora za afya karibu na makazi.
Kwa upande wake, Mgeni Rasmi Dr. Daniel Ringo mwakilishi wa Mganga mkuu wa wilaya ya Temeke, ameelezea umuhimu wa kambi hiyo ya uchunguzi na tiba na naman ilivyoweza kunufaisha wakazi wa wilaya ya temeke na maeneo ya karibu. Dr Ringo amewapongeza madaktari bingwa walioshiriki katika kutoa huduma za kibingwa na bingwa bobezi
“tumeona commitment ya ajabu sana, kwakweli madaktari bingwa wa temeke na wa Yombo vituka kwa kweli nawapongeza sana” na kuongezea kuwa “uwepo wa klinki hizi za kibngwa zinawaongezea uwezo madaktari waliopo katika vitu afya”
Aidha mkazi wa Yombo vituka, Bw Urassa ameshukuru jitihada za Mhe Rais kwa kuweza kuwafikia wananchi na huduma bora za afya bila wao kuzitafuta au kuhangaikia.