Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi akizuzungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga ofisini kwake
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakichukua matukio mbalimbali
Na Oscar Assenga, TANGA
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kuwakamata raia wawili wa Kenya ambao wamekuwa wakifanya uhalifu wa kuiba pesa na mali za watu kutoka kwenye magari yao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi alisema kukamatwa kwa raia hao kunatokana na operesheni mbalimbali za kukabiliana na uhalifu mkoani humo.
Alisema kwamba watu hao wamekuwa wakivizia watu wanakienda kuchukua fedha zao benki wakienda kupaki sehemu wanafungua magari na kuchukua fedha .
Kamnada huyo alisema watuhumiwa hao walikamatwa saa tatu na nusu asubuhi eneo la Barabara 13 Ngamiani Kati na Tarafa ya Ngamiani Kati wilaya ya Tanga walikamatwa watuhumiwa hao wawili.
Aliwataja walikamatwa ambao ni raia wa Kenya ni Idrisa Mussa Kasimu (24) fundi umme raia wa Kenya na Samweli Kimath Mwenda (35) mfanyabiashara raia wa Kenya ambao watuhumiwa hao walikuwa wanatumia gari aina ya IST yenye namba zaa usajili T931 CVS ambao walikuwa wanalitumia kutekeleza wizi huo.
Aidha alisema watu hao walikamatwa na kufanyiwa upekuzi na gari walilokuwa nalo na kufanikiwa kukutwa na rimoti rangi nyeusi ambazo hutumika kutolea alamu za magari,rimoti rangi ya kijivu ambayo hutumika kutoa lock za magari.
Alisema pia wakimatwa na rimoti ndogo rangi jeusi ambalo hutumika kufungulia mageti,simu tatu smart phone na simu ndogo na vitambulisho mbalimbali ambavyo vilikuwa vinawasaidia kutekeleza uhalifu huo.
Kamanda huyo alisema katika mahojiano watuhumiwa hao walikiri kufanya makosa hayo katika maeneo mbalimbali lakini kosa lilithibitika ni moja ambalo tayari wameshawafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.