Naibu Mkurugenzi Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Fatma Kabole akizungumza na wahudumu wa afya kuhusu utumiaji wa kauli nzuri kwa wagonjwa katika Kikao cha kujadili utekelezaji wa Mfumo wa M-mama uliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Wahudumu wa afya na Madereva wakimsikiliza Naibu Mkurugenzi Idara ya Kinga na elimu ya afya Fatma Kabole (hayupo pichani) katika Kikao cha kujadili utekelezaji wa Mfumo wa M-mama uliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Mkuu wa kitengo cha Tehama Mohamed Al-Mafazy akitoa elimu kwa madereva na wahudumu wa afya kuwa karibu na vituo vyao ili kupunguza vifo kwa mama wajawazito katika Kikao cha kujadili utekelezaji wa Mfumo wa M-mama uliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Afisa Mdhamini wa Wizara ya Afya Pemba Khamis Bilal Ali akifunga Kikao cha kujadili utekelezaji wa Mfumo wa M-mama uliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Afisa Programu kutoka Shirika la Pathfinder Abdallah Isaa akitoa mafunzo kwa wahudumu wa afya juu ya mfumo wa M-mama katika Kikao cha kujadili utekelezaji wa mfumo huo uliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Raha . (Picha na Rahima Mohamed HABARI MAELEZO).
……….
Asya Khamis – MAELEZO ,20/09/2023.
Wafanyakazi wa Kitengo cha Afya pamoja na Wakunga wametakiwa kutumia kauli njema kwaakinamama wajawazito ili kuondoa kero wakati wa kupatiwa huduma katika vituo vya afya.
Hayo yameelezwa na Naibu Mkurugenzi Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Bi Fatma Kabole katika Kikao cha kujadili Utekelezaji wa Mfumo wa M-mama uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Amesema hatua kali zitachukuliwa kwa mfanyakazi ambaye atabainika kutoa kauli chafu kwa wamama wajawazito ambazo zinakwenda kinyume na maadili ya sheria ya afya katika vituo vya kutoa huduma hiyo .
Aidha amewataka washiriki wa mkutano huo kuwa mabalozi kwa wengine katika kuhakikisha wanasambaza elimu hiyo waliyopatiwa ili kupunguza vifo vya wamama wajawazito pamoja na watoto wachanga.
Hata hivyo, amewataka washiriki hao kuendelee kushirikiana kwa pamoja katika kutokomeza vitendo viovu vinavyofanyika vituoni mwao.
Nae Mkuu wa Kitengi cha Tehama ( ICT) kutoka Wizara ya Afya Mohammed Al Mafazy, amewaomba madereva wa ambalesi kuwa karibu na vituo vyao ili kutoa mashirikiano kwa wahudumu wa afya kwa lengo la kuokoa maisha ya mama na mtoto wanapopatiwa rufaa ya kwenda katika hospitali kuu Mnazimmoja
Kwa upande wake Bi Fatma Abdulla Mohamed kutoka Hospital ya Mnazimmoja ameeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kuzalishia akinamama wajawazito .
Mkutano huo wa siku moja umewashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Wakunga wa Wilaya, Maafisa Wadhamini, EGA, Madereva wa Ambalesi na Wahasibu kutoka Wizara ya Afya