Na Ahmed Mahmoud
Chuo cha Uhasibu Arusha IAA kimeanzisha mahusiano na Jeshi la Polisi kupitia Chuo cha Polisi Moshi CCP ikiwa na Lengo la kutoa kozi za fani nne kwa Askari wa Jeshi hilo.
Akiongea na Waandishi wa Habari mapema Jijini Arusha kuelezea mafanikio ya Chuo hicho, Mkuu wa Chuo hicho Prof. Eliaman Sedoyeka amesema kozi ni sehemu ya kulipeleka Jeshi hilo kidigitali.
Amesema kwamba Sasa hivi wameanzisha rasmi mahusiano na Jeshi la Polisi ambapo wanaenda kutoa kwa kushirikiana na chuo chao cha Moshi kutoa Kazi nne katika maeneo ya teknolojia ya ulinzi sanjari na ulinzi mtandao.
Kwa mujibu wa Prof. Sedoyeka wataenda kutoa Shahada ya Usalama wa kimtandao na Shahada uzamili katika fani ya mkakati wa mafunzo ya ulinzi (strategy study) na Shahada ya pili ya Usalama (Peace Security).
Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 chuo hicho imepata mafanikio na kimeanzisha ujenzi wa majengo ya utawala na mabweni katika mikoa ya Arusha Manyara na Songea ili kuongeza udahili sanjari na kuongeza idadi ya waalimu kufikia 334 na wanafunzi wa Shahada ya kwanza 3691 mwaka 2018/19 hadi kufikia 13716 Juni mwaka huu.
Hata hivyo pia imeongeza wanafunzi wa Shahada ya pili kutoka 178 Hadi 2069 katika mwaka 2018/19 Hadi kufikia juni mwaka huu,na chuo kimepata faida ya takribani billion 45.273 katika mwaka wa fedha 2022/23.
Vile vile chuo hicho kimeendelea kuboresha kituo atamizi kwenye fani za Benki na na kuzalisha makampuni ya wanafunzi mawili Mood Uji na kido ambapo kwa mwaka ujao wanatarajio kuongeza zaidi
Amesema kwamba wanatarajia kukamilisha ujenzi wa hosteli za wanafunzi sanjari na mikakati mipya kupitia mradi wa heat unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 21 ambapo katika hizi zinaenda kuboresha chuo hichi cha Arusha na kuboresha miundombinu katika campus ya Manyara na kujenga cumpus mpya Songea.
Alisema kwamba Sasa hapa Arusha ni ujenzi wa kituo cha kimkakati cha ICT na Lengo letu sisi ni kuhakikisha kwamba kwa kuwa sisi ni chuo cha Uhasibu na mambo ya fedha na ujasiriamali lakini sisi pia tupo chini ya Wizara ya fedha na tunawajibika kutoa msaada wa kitaalamu kwa sekta nzima ya kifedha.
Kwa mujibu wa Prof Sedoyeka amesema mwaka ujao wa fedha wanaenda kuboresha na kukamilisha miradi ya Ujenzi katika cumpus za Babati Dodoma na kuanza Ujenzi cumpus ya Songea sanjari na kuongeza ubora wa mfumo wa elimu inayotelewa chuo ni hapo (ISO 21001).