Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmed Okeish akimjulia hali mtoto aliyepatiwa matibabu katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kutoka nchini Saudi Arabia wakati wa ziara yake kutembelea kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmed Okeish akisalimiana na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kutoka nchini Saudi Arabia wakati wa ziara yake kutembelea kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na watalamu wa afya kutoka Saudi Arabia na wenzao wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akitembelea moja ya chumba cha upasuaji wa moyo kuangalia huduma zinavyoendelea wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Mwakilisha wa Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Leonce Bilauri akimpatia zawadi kwa kazi nzuri waliyoifanya Afisa Uuguzi kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kutoka nchini Saudi Arabia Reef Alrokaeini wakati balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmed Okeish alipotembelea kambi ya matibabu inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmed Okeish akimpatia cheti mzazi ambaye mtoto wake amefanyiwa upasuaji wa moyo na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia Merciana Wiston wakati balozi huyo alipotembelea kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia wakifuatilia wakati balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmed Okeish alipotembelea kambi ya matibabu ya moyo kwa watoto inayoendelea katika Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam
.……………………..
Na Sophia Kingimali
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) imeishukuru serikali ya Saudia Kwa kuendeleza ushirikiano na nchi katika sekta ya afya ambapo imesaidia upasuaji wa moyo Kwa watoto.
Akizungumza Leo Septembea 13 wakati akiwaanga madaktari kutoka Saudia waliokuweo nchini Kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa watoto mkurugenzi mtendaji wa JKCI Peter Kisenge amesema ushirikiano huo umeweza kuzaa matunda Kwa nchi.
Amesema tangu wameanza kutoa huduma za upasuaji nchini 2019 wameshahudimia wagonjwa 439.
“Hii imefanyika kutokana na undugu uliopo Kati ya serikali ya Saudia na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambapo rais Dkt Samia. Amekua mstari wa mbele kudumisha uhusiono huu”amesema Kisenge
Amesema madaktari ambao waliokuweo wameweza kusaidia watoto 30 ambao wamekuwa na furaha baaada ya kupatiwa huduma.
Amesema uwepo wa madaktari hao nchini licha ya kutoa huduma Kwa watoto lakini pia umesaidia kutoa elimu Kwa madaktari nchini.
Amesema tangu serikali ya saudia walipoanza kutoa huduma hapa nchini zàidi ya bilioni 3.5 zimeweza kupatikana.
Aidha Dkt Kisenge ameishukuru serikali Kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kutolea huduma ambapo imesaidia Kwa kiasi kikubwa utolewaji wa huduma za upasuaji nchini.
Kwa upande wake barozi wa Saudia nchini Yahya Ahmed Okeish amesema wataendeleza uhusiano na serikali ya Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya.
Amesema wataendelea kuleta madaktari bigwa nchini ili kusaudiana na madaktari wa hapa nchini ambapo Kwa Sasa watakua wanakuja mara mbili Kila mwaka.
Nae kaimu mkurugenzi idara ya Mashariki na Kati kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Leonce Bilauri ameipongeza serikali ya Saudia Kwani wamekuwa wakishirikiana na serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu maji,barabara,kilimo na sekta ya Afya.
Amesema serikali itaendeleza ushirikiano huo Kwani umesaidia kurudisha tabasamu Kwa watanzania lakini kuokoa Fedha nyingi ambazo ziingetumika kupeleka wagonjwa kutibiwa nje.
Aidha nae Dkt Angela ametoa Rai Kwa serikali ya Saudia kurudi nchini mara Kwa mara Kwani watoto zàidi ya 500 wanasubiri upasuaji
Nae mzazi ambae mtoto wake amenufaika na huduma hiyo bi Janeth ameipongeza serikali Kwa kujali wananchi wake na kuwapunguzia gharama za matibabu lakini pia kuokoa Maisha ya watoto.
Aidha Janeth amesema kuwa idadi ya watoto wanaugua ugonjwa wa moyo ni wengi hivyo serikali iendeleze ushirikiano huo ili kusaidia wananchi.