Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Slaam
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Mdau wa Utamaduni na Sanaa Bi. Belinda Mlingo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kurasimisha utamaduni wa Mtanzania katika eneo la jando na unyago.
Kikao hicho kimefanyika Septemba 13, 2023 katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es salaam ambapo wamejadili umuhimu wa kurasimisha elimu ya jando na unyago hatua itakayosaidia kurekebisha tabia za vijana kulingana na mila na desturi za kiafrika ili zitumike kibishara ndani na nje ya Tanzania.
Aidha, wamejadili pia namna ya kubidhaisha mazao ya Sanaa ya Tinga Tinga ili itumike katika kutambulisha Tanzania kimataifa pamoja na kujenga sehemu ya watu kuona vitu vya asili (Theam Park) ambayo itasaidia kukuza utalii wa liutamaduni ambao ni kivutio cha watalii wengi kuja nchini.
Kwa upande wake Mdau wa huyo Bi. Belinda Mlingo amesema yeye ni Mwana Dispora ambaye amejikita kurasimisha mila na desturi za mtanzania ikiwemo elimu ya jando na unyago ili kuwa na jamii inayozingatia Sheria za asili ambayo ni msingi wa mil ana desturi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa nchini Dkt. Emmanuel Ishengoma ambaye ndiye anasimamia sekta hiyo inayobeba kitambulisho kikubwa cha taifa kupitia kazi za Sanaa.
Utamaduni wa mtanzania ni wa kipekee unahusisha aina ya vyakula, mavazi, vitu mbalimbali wanavyotumia, imani zao, makazi, mapokeo yao na hata mahisiano na malezi ya watoto. Tofauti hiyo ndiyo inawavuta watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuona aina na upekee wa watu wa Tanzania.