Mkurugenzi wa Skuli ya Trifonia Grace Peter Myamba akikabidhi vitu mbalimbali kwa Wazee wa Kituo cha kulelea Wazee Welezo kushoto ni Afisa Wazee Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee Zanzibar Pili Sadala Mussa.
Mwakilishi wa Kamati ya Wazee Skuli ya Trifonia Dorice Mwakasendo akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wazee wanaoishi nyumba za kutunzia Wazee Welezo ikiwa ni mrejesho wa Skuli hiyo kwa jamii kuelekea kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.
……………………………..
Na Rahma Khamisi Maelezo 13/9/2023
Uongozi wa Skuli ya Trifonia umesema utaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwajali na kuwathamini wazee wasiojiweza nchini.
Aakizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa Vitu mbalimbali kwa wazee katika Kituo cha Kulelea Wazee Welezo, Mkurugenzi wa Skuli hiyo Grace Bernad amesema hatua hiyo itasaidia kuwafanya wazee hao kujiona wapo sawa na watu wengine.
Alisema msaada huo utawafajiri wazee hao na kuwasaidia katika mahitaji yao ya kila siku .
Aidha alieleza kuwa wamefaraijika kuona wazee wanaotunzwa katika nyumba hizo na Serikali ya Mapinduziaya Zanzibar kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee zinaendelea vizuri na kuahidi kusaidia wazee hao mara kwa mara .
Hata hivyo wamewashauri wadau ,na taasisi zenye uwezo kuwapitia na kuwafariji wazee hao kwa kupatia Misaada mbalimbali ya kujikimu katika mahitaji yao
“Tumetoa msaada huu kwa lengo la kuwafanya wazee hawa kuona kuwa bado tunawajali na kuthamini nguvu zao kabla ya uzee kwani na wao walikuwa kama sisi “,alisisitiza.
Nae Mkuu wa Kituo cha kulelea Wazee wasiojiweza Welezo Khamisi Ali Haji amesema kuwa hatua iliyo chukuliwa na Skuli hiyo ni njema kwani wameisaidia Serikali katika kutimiza majukumu yao.
Hata hivyo walishukuru na kupongeza ujio wa Skuli hiyo katika kituo hicho na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuunga mkono jitihada hizo.
Katika Msaada huo Wazee hao walipokea vitu mbalimbali ikiwemo dawa ,unga ,sukari ,mafuta na mashuka kutoka kwa Uongozi wa Skuli ya Trifonia ikiwa ni mrejesho kwa jamii kuelekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.