Nibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara mara baada ya kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mara.
Baadhi wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Manispaa ya Musoma mkoani Mara wakimfurahia Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mara.
Mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Manispaa ya Musoma mkoani Mara akimfurahia Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuzungumza na walengwa wa Manispaa hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Mara.
……
Na Lusungu Helela-Musoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewapongeza walengwa wa naoratibiwa na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Manispaaa ya Musoma Mkoa wa Mara kwa ubunifu katika kujikwamua na wimbi la umaskini.
Mhe. Ridhiwani amesema ujenzi wa barabara ya Bwire katika Manispaaa ya Musoma na Kaya nne zilizojikwamua kwa kujenga makazi bora kupitia fedha zinazotolewa na TASAF ni mfano wa kuigwa na ndiyo lengo mahususi la uwepo wa mfuko huu.
“Maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona walengwa wote wanajikwamua na wimbi hili la umaskini na ndiyo maana ameongeza fedha katika mfuko huu ili ziweze kumfikia kila mlengwa kwa wakati” alisistiza Mhe. Ridhiwani.
Aidha, Mhe. Kikwete amesema Serikali iliamua kutumia mfumo wa malipo ya kielektoni katika kufanya malipo kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kuziba mianya ya upotevu wa fedha lakini baadhi ya Waratibu wa Mfuko wameshindwa kuutumia ipasavyo na hivyo kuleta malalamiko makubwa kwa walengwa wa Mkoa wa Mara kwani wengi wao ni wazee ambao hawana simu na hawajui kusoma na kuandika.
Hivyo, Mhe, Kikwete amewataka Waratibu wa TASAF kutoka Makao Makuu kuhakikisha walengwa wote katika Mkoa wa Mara wanalipwa kwa njia ya malipo ya fedha taslimu ili kuondoa malalamiko yaliyopo na yenye kuleta chuki dhidi ya Serikali ya Mhe. Samia Suluhu Hassan.
“Ninatoa maekelezo haya kwa kuwa malalamiko ya walengwa wengi wa TASAF katika ngazi ya Wilaya na Mkoa huu yanahusu Waratibu wa Mfuko kushindwa kulipa malipo ya walengwa kwa mfumo wa kielektroni (e-payment) kwa wakati kutokana na dosari ya taarifa zao kwenye mfumo” alisema Mhe. Kikwete.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe. Dkt. Khalfan Haule amesema tangu walengwa walipoanza kulipwa kwa njia ya mfumo wa Kielektoni kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na hali duni za wanufaika na kushindwa kumudu vigezo vya matumizi ya mfumo.
Mhe. Kikwete amezungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.