Picha ya pamoja |
Picha ya pamoja |
========================================
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi umeshiriki kwenye Maadhimisho ya
Siku ya Umoja wa Afrika yaliyofanyika jijini Lilongwe tarehe 9 Septemba, 2023.
Katika kutangaza Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania ulitumia fursa hiyo kutangaza fursa za Uwekezaji, kuhamasisha matumizi ya
Lugha ya Kiswahili na kutangaza vivutio vya Utalii kwa kuonesha Filamu ya The
Royal Tour.
Kadhalika Ubalozi ulishirikiana na
Watanzania Diaspora wanaoishi Malawi kuonesha Utamaduni wa Tanzania ikiwemo vyakula vya asili.
Banda la Ubalozi wa Tanzania lilitembelewa na wageni wengi ambao walipendezwa na vyakula vya asili kutoka Tanzania.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Simplex Chithyola.