Na Sophia Kingimali
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Husein Ali Mwinyi amewataka wadau kuendelea kuchangaa fedha Kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT).
Akizungumza katika mkutano wa harambee uliofanyakia katika mkutano wa pembeni wa jukwaa la mifumo ya chakula Afrika AGRF uliolenga kuhamasisha washirika na wadau kusaidia mpango wa BBT Rais Dk. Mwinyi amesema, kumekuwa na utashi wa kisiasa unaokua kwa kasi Barani Afrika hususani Tanzania unaolenga kuwawezesha vijana na wanawake katika kilimo biashara.
Amesema, utashi huo unaonekana kufuatia juhudi mbalimbali ikiwemo kupitishwa mikata ya tamko la mpango wa utekelezaji wa vijana, kunzishwa kwa dawati la vijana katika mpango mpya wa ushirikiano wa pamoja na uwezeshaji mpango wa BBT.
Rais Dk. Mwinyi amesema, hatua ya uwezeshaji wa mradi wa BBT utaongeza ajira kupitia mfumo wa chakula ambapo serikali imeandaa mikakati shirikishi na kutekeleza mipango ya kusaidia vijana na wanawake katika sekta ya kilimo biashara.
“Kutokana na kukua kwa mifumo ya kidigital inayosimamia mabadiliko ya uchumi wa dunia kumekuwa na ongezeko la kasi kwa vijana kuwa sehemu ya ukuaji wa uchumi Afrika kupitia kilimo.
Amesema hata hivyo bado kuna changamoto ya ushiriki mdogo wa vijana na wanawake katika sekta za kilimo na uvuvi kutokana na upatikanaji mdogo wa rasilimali za uzalishaji, ujuzi na ukosefu wa mitaji.
Amesema vijana wanayo hamu ya kuwekeza sehemu zenye matokeo ya haraka.
Rais Dk. Mwinyi amesema ili kufikia mafanikio yapo maeneo yanahitaji ufumbuzi ikiwemo uptikanaji wa huduma za kijamii vijijini ili kupunguza wimbi la vijana ambao wanao uwezo wa kushiriki katika kilimo kuhamia mjini.
“Pia ni mujimu kumaliza tatizo la kukosekana kwa masoko, vikwazo vya kimazingira na mabadilioo ya tabia nchi, kukosekana kwa miundombinu ya uzalishaji na kutafuta ufumbuzi katika uwekezaji wa teknolojia,”amesema.
Amesema, uwezeshaji wa vijana na wanawake katika sekta hiyo ni ufunguo wa milango ya ajira, kupunguza umaskini na chanzo cha matokeo ya uzalishaji wa chakula na ongezeko la thamani.
Rais Dk. Mwinyi amesema kutokana na hali hiyo serikali ya Tanzania imejidhatiti katika kuwawezesha vijana na wanawake kufikia malengo yao, ikiwemo kuwapo na mazingira wezeshi katika kilimo biashara.