Na John Walter-Manyara
Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ameanzisha mpango wa kusikiliza kero za wananchi kwa kuwafuata kwenye Mitaa na vijiji vyao kupitia ofisi inayotembea (Mobile office) ili waweze kuwafikia kwa wingi zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo septemba 6,2023 amesema kuanzia kesho alhamisi septemba 7,2023 ataambatana na idara, taasisi zote za serikali zilizopo katika wilaya ya Babati kusikiliza na kuzitatua kero zote zilizopo.
Pia, DC Twange amewataka watumishiwote wa serikali kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita katika kuwahudumia wananchi.
Amewataka Madiwani, Wenyeviti wa mitaa, vijiji na watendaji wa serikali katika kata vijiji na mitaa kuwahimiza wananchi kufika katika maeneo mkutano utakapofanyika.
Twange amewasihi wananchi kutoa kero, changamoto na matatizo yao bila hofu yoyote kwa kuwa serikali ipo kwa ajili yao.