Waziri wa Ujenzi, Mhe Innocent Bashungwa, akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala, wakati alipotembelea ofisi za Wakala huo, jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Mha, Balozi Aisha Amour.
Waziri wa Ujenzi, Mhe Innocent Bashungwa, akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mha ,Balozi Aisha Amour ,wakati alipotembelea ofisi za Wakala wa Ufundi na Umeme Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi Mha, Balozi Aisha Amour, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) wakati alipotembelea ofisi za wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala, akizungumza na Menejimenti ya Wakala huo wakati Waziri wa Ujenzi Mhe Innocent Bashungwa (katikati) alipotembelea ofisi zao jijini Dodoma.
Menejimenti ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (hayupo pichani) wakati akizunguza katika kikao kazi na Menejimenti ya Wakala huo, jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa, akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) katika kikao kazi kati ya Menejimenti ya Wakala huo na Waziri huyo, jijini Dodoma.
……..
Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa, ameutaka Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kuja na mikakati itakayouwezesha Wakala huo kufanya kazi kibiashara ili kuleta tija katika utendaji kazi wake.
Akizungumza mara baada ya kukutana na Menejimenti ya wakala huo Mhe Bashungwa amesema huu sio wakati wa TEMESA kulalamika na kusononeka, ni wakati wa kujali wateja na kushindana katika soko ili kupata wateja wengi na kuhudumia sehemu kubwa ya jamii kwenye upande wa umeme, eletroniki, mitambo uendeshaji wa vivuko na utengenezaji wa magari.
‘’Namshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha za kutosha za kusimamia miradi yenu, hivyo hakikisheni mnazitumia fedha hizo kwa uaminifu na uadilifu na kuhakikisha miradi ya ujenzi mnayoendelea nayo hususani ya vivuko na huduma za ufundi wa umeme na magari inakamilika kwa wakati,’’amesema Mhe. Bashungwa.
Waziri huyo wa Ujenzi amewataka wafanyakazi wote wa TEMESA kufanya kazi kwa mtazamo chanya utakaovutia jamii kubwa ya Watanzania kutumia huduma za TEMESA ambazo zitakuwa bora, za uhakika na za kuaminika badala ya kwenda kupata huduma hizo kwenye taasisi zingine.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ujenzi, Mhandisi Balozi Aisha Amour, amemhakikishia Waziri wa Ujenzi kuwa TEMESA iko kwenye mkakati wa mabadiliko katika utendaji na ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha mapato yote yanayopatikana yanakusanywa kwa wakati.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Lazaro Kilahala, amesema kuwa maelekezo yote na miongozo iliyotolewa na Wizara itafanyiwa kazi na kuelekezwa kwa watumishi wote wa Wakala huo nchini.
Waziri Bashungwa alikua katika ziara ya kukutana na Menementi ya TEMESA ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Mhe Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa Waziri wa Ujenzi.