Na John Walter-Manyara
Vituo vingi Mkoani Manyara havitoi huduma kutokana na ukosefu wa mafuta huku kukishuhudiwa foleni Kubwa ya magari,pikipiki na bajaji kwenye kituo kimoja mjini Babati.
Mjini Babati baadhi ya watu walionekana wakijaza mafuta wakiyatia ndani ya chupa za maji na madumu.
Katika wilaya ya Hanang’, Katesh ni Kituo kimoja pekee kilikuwa kinatoa huduma Septemba 4.
Afisa Biashara Halmashauri ya mji wa Babati Fue Chedieli amesema Vituo vyote vilivyopo Mjini hapo vimeishiwa Mafuta na kwamba kituo kimoja pekee ndicho kinachotoa huduma kuanzia asubuhi ya leo.