Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajii wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Loy Mhando (kulia) na Afisa Usajili Bi. Gift Wazingwa (kushoto), wakifuatilia maombi ya Usajili wa Alama ya Biashara kwa mdau aliyefika katika banda la Taasisi hiyo ( hayupo pichani) leo tarehe 5 Septemba, 2023, katika Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) , jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo lililoanza leo tarehe 5 litahitimishwa Septemba 8, 2023.
Afisa Usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Gift Wazingwa, akiwahudumia wadau mbalimbali waliofika katika banda la Taasisi hiyo leo Septemba 5, 2023 lililopo nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), ambako Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika linafanyika kuanzia tarehe 5-8 Septemba, 2023 .
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Loy Mhando (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi hiyo Bi. Roida Andusamile (kushoto) na Bi. Gift Wazingwa (kulia), wanaotoa elimu katika banda la BRELA sambamba na Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo lililoanza leo tarehe 5 litahitimishwa Septemba 8, 2023.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Loy Mhando (kulia) akiwa katika banda la Taasisi hiyo nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambako Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika linafanyika kuanzia tarehe 5-8 Septemba,2023 jijini Dar es Salaam. Aliyeketi katikati ni Afisa Usajili Bw. Gift Wanzigwa na kushoto ni mdau aliyefika kupata huduma ya Usajili wa Kampuni Bw. Lucas Mlehu.
……………………………….
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inashiriki katika Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (Africa Food Systems Forum – AGRF), kwa kutoa elimu ya urasimishaji biashara kwa washiriki wa Jukwaa hilo.
Banda la BRELA ambalo lipo ndani ya banda la Wizara ya Viwanda na Biashara, linatoa elimu juu ya huduma zote za BRELA ikiwa ni pamoja na Usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Kampuni, Alama za Biashara na Huduma, Utoaji Hataza pamoja na Leseni za Viwanda na za Biashara Kundi “A”.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Jukwaa hilo leo Septemba 5, 2023 Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amewataka Watanzania kutumia Jukwaa hilo la AGRF linaloendelea Jijini Dar es Salaam kama fursa ya kuijulisha Dunia rasilimali zilizopo nchini na namna gani Watanzania watashiriki kuzitumia ili waweze kufanya biashara na mataifa mengine Duniani na hasa biashara ya chakula kwakuwa Dunia inatarajia kuwa na watu Bilioni Tisa ifikapo mwaka 2030, ambapo kwa Bara la Afrika inakadiriwa kufikia watu bilioni mbili, na Tanzania watu milioni 80 ambao wote wanahitaji chakula.
“Kufanyika kwa Jukwaa hili hapa nchini, kutatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima kwakuwa kilimo kinahitaji fedha, na pia uwekezaji wa kumsaidia mkulima mdogo ama mkubwa, hivyo jukwaa hili limewaleta pamoja wawekezaji mbalimbali ambao watawezesha wakulima kwa mitaji”, amefafanua Mhe. Bashe.
Jukwaa hilo linalofanyika kwa siku nne limeandaliwa na Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (Africa Food Systems Forum), ambalo limewakutanisha wadau kujadili kwa pamoja hatua za kuboresha kilimo na mifumo ya chakula barani Afrika.