Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo kuhusiana na Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika AGRF unaotarajia kuanza tarehe 5-8 Mwezi huu katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Mikutano cha Julius Nyerere JNICC Ephrahim Mafuru akifafanua mambo kadhaa kuhusu maandalizi ya mkutano huo.
…………………….
Na Sophia Kingimali
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo kuhusiana na Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika AGRF, unaotarajia kuanza tarehe 5-8 Mwezi huu katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.Na Sophia Kingimali
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wananchi kutumia fursa zitakazopatikana katika mkutano mkuu wa jukwaa la mifumo ya chakula Afrika AGRF ili kuboresha shughuli za kilimo
Amesema mkutano huo utaleta matokeo muhimu katika uendelezwaji wa mfumo wa chakula Afrika , ukuzaji wa sekta ya utalii,biashara na uwekezaji na kukuza teknolojia mpya.
“Jukwaa la mfumo wa chakula la Afrika(AGRF) ni jukwaa kuu la kilimo linalowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo ili kujadili na kuchukua hatua za kiutendaji katika kuboresha njia za upatikanaji na usalama wa chakula na lishe kwa ujumla,”amesema Chalamila
Chalamila amesema mkutano huo utawakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji, wawekezaji, na wafanyabiashara.
Amesema wakazi wa Dar es Salaam wanapaswa kuchangamkia fursa zitakazotokana na mkutano huo kwa lengo la kuongeza uzoefu na kujifunza teknolojia za kisasa ili kutimiza malengo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kulisha dunia.
Aidha Chalamila amewataka wakazi hao kudumisha usalama, ukarimu na usafi ili kuweka taswira ya nchi vizuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Mikutano cha Julius Nyerere JNICC Ephrahim Mafuru amesema serikali inatatarajia kupokea wageni zaidi 3000 wa masuala ya kilimo jumla ya sh. Bilioni 12.5 zimetolewa kwa ajili ya maandalizi ya mkutano (AGRF).
Amesema JNICC wamejipanga kuwahudumia wageni hao kwa kutenga jumla ya kumbi 27 ambazo zote maandalizi yake yamekamilika.
“Mchango wa kituo katika mnyororo wa thamani hivyo serikali kwa kushirikiana na AGRF imejipanga kwa bajeti ya bilioni 12.500 na fedha hizo ni maandalizi ya mkutano ambazo zitaingia katika mnyororo wa thamani wa maandalizi na gharama za kuuendesha mkutano huo,”amesema.
Aidha Mafuru ameongeza kuwa zaidi ya vyumba 2600 vya hoteli vimeandaliwa kwa ajili ya wageni hao hivyo amewaomba Watanzania kuwakarimu wageni hao kwani mchango wao ni mkubwa kwa taifa.
Hata hivyo Mafuru amewataka wajasiriamali watakaopata nafasi ya kushiriki mkutano huo watumie fursa hiyo kukutana na wajasiriamali kutoka nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu.
Mkutano huo unatarajia kufanyika nchini Septemba 05 hadi 08,mwaka huu katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na utazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan