Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Comred Ally Mandai (kushoto) akimkabidhi Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Comred Bi. Fratta Katumwa Makablasha ya Muongozo wa Mafunzo kwa Viongozi wa Chama kuanzia ngazi matawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa, (kulia) ni Katibu wa Siasa na Uenezi Chama Cha CCM Mkoa wa Dar es Salaam Comred Ally Bananga.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Comred Ally Mandai (kulia) akimkabidhi Katibu wa Siasa na Uenezi Chama Cha CCM Mkoa wa Dar es Salaam Comred Ally Bananga Makablasha ya Muongozo wa Mafunzo kwa Viongozi wa Chama kuanzia ngazi matawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ajili ya kuwapatia Makatibu Kata Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala katika kikao kazi kilichofanyika Agosti 30, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Comred Mtiti Jirabi Mbassa akizungumza jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha Makatibu Kata ya Jumuiya ya Wazazi kwa ajili kujadili mipango mbalimbali pamoja na kupokea maelekezo ya utekelezaji.
Kaimu Katibu / Emma Kata ya Ilala Bi. Firdaus Sija Karibu (kulia) akipokea kablasha la muongozo wa mafunzo kwa viongozi wa Chama kuanzia ngazi matawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa kutoka kwa Katibu wa Siasa na Uenezi Chama Cha CCM Mkoa wa Dar es Salaam Comred Ally Bananga.
Makatibu Kata wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha CCM wakiwa katika kikao kazi.
….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala leo Agosti 30, 2023 imepokea makablasha ya muongozo wa mafunzo kwa viongozi wa Chama kuanzia ngazi matawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa kutoka kwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa Comred Ally Mandai.
Akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala baada ya kukabidhi Makablasha ya Muongozo wa Mafunzo kwa Viongozi wa Chama kuanzia ngazi matawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa Makatibu Kata wa Jumuiya ya Wazazi, Katibu wa Siasa na Uenezi Chama Cha CCM Mkoa wa Dar es Salaam Comred Ally Bananga, amesema kuwa wajumbe wa kamati tendaji ngazi Kata wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kulinda na kusimamia kiukamilifu katiba, kanuni na miongozo ya jumuiya ya wazazi katika Taifa na ndani ya chama cha mapinduzi.
Hata hivyo Comred Bananga amempongeza Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Comred Mtiti Jirabi Mbassa kwa kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta maendeleo yenye tija katika Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala.
“Ilala wana Katibu wa Wazazi, Katibu huyu ni bora sana, kazi hii unaiweza na muda sio mrefu unaweza kujikuta wewe sio wa Ilala, nina mwezi mmoja nimeona wewe ni mchapa kazi” amesema Comred Bananga.
Naye Comred Ally Mandai amesema kuwa ni muhimu kufata miongoni kupitia mafunzo ya viongozi yaliyotolewa ili kuleta tija na ufanisi katika utendaji.
Awali Comred Bananga na Mandai walimkabidhi Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Comred Bi. Fratta Katumwa muongozo ya mafunzo kwa viongozi wa chama kuanzia ngazi ya matawi, kata, Wilaya, Mkoa na Taifa.
Hata hivyo Katibu wa Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Comred Mtiti Mbassa Jirabi amewakumbusha Makatibu Kata Kufanya vikao kwa kuzingatia kanuni na taratibu.
Comred Mbassa amesema kuwa ni muhimu kufanya vikao vya kikanuni kuanzia ngazi ya matawi ili kuleta ufanisi katika utendaji wa Jumuiya ya Wazazi.
“Kuna utaratibu wa mikutano ya Jumuiya ya wazazi katika kila tawi, upo mkutano mkuu wa wazazi wa tawi, mkutano wa wanachama wote, kamati ya utekelezaji wa wazazi, kamati utendaji wazazi ya tawi” amesema Comred Mbassa.
Amefafanua kuwa mkutano mkuu wa tawi ni kikao kikuu cha Jumuiya ya Wazazi katika tawi, huku akieleza kuwa mkutano mkuu wa wazazi wa tawi utafanya mkutano wa kawaida mara moja kwa mwaka.
“Ndugu zangu wajumbe wa kamati tendaji ngazi ya kata nendeni mkasimamie hayo, huku kamati ya tendaji ya wazazi Wilaya itashuka kuona utendaji kazi kwa mujibu wa Kanuni kama utekelezaji wake umefanyika” amesema Comred Mbassa.