Diwani wa kata ya Kisima halmashauri ya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe.Wilfred John amewaongoza wakazi wa kata hiyo Katika msalagambo kusafisha pori na vichaka katika eneo kulikopangwa kufanyika ujenzi wa shule mpya Sekondari ya kata ya Kisima.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo Mhe.Diwani Huyo amewaeleza wananchi kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samiha Suluhu Hassani imetoa kiasi cha shilingi Milioni 850 kwa ajiri ya ujenzi wa shule hiyo ambayo ujenzi wake utaanza hivi karibu ikilenga kusaidia wanafunzi kuondokana na ulazima wa kutembea umbali mrefu
Mbali na amewataka wananch kuendelea kuunga Mkono uongozi wa Serikali hasa kushiriki kwa kujitolea nguvukazi kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao pia uboreshwaji wa huduma.
“Niendelee kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mbalimbali hasa mkuu wetu wa wilaya ya Same Mhe. Kasilda Mgeni kwa kazi kubwa anayoifanya kuendelea kusimamia Miradi mbalimbali hapa Kwenye wilaya yetu ya Same na wananchi sisi ni mashahidi tunaona kazi kubwa ya maendeleo na kwa kiasi kikubwa asilimia kubwa ya miradi inaenda kukamilika kwa wakati”. Alisema
Amewataka pia wananchi hao kuendelea kutekeleza maelekezo ya serikali hasa kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo wilayani humo hasa mkazo unaotolewa Mara kwa mara na Mkuu wa wilaya kusisitiza kilimo cha Mkonge na Parachichi kuendana na ushindani wa kibiashara Kwenye mazao hayo.