NA STEPHANO MANGO, NAMTUMBO
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM (Uvccm) wilaya ya Namtumbo George Luambano amewataka vijana kuwa wazalendo wa nchi yao na kuachana na tabia ya kujihusisha na mambo ambayo hayana tija yoyote kwa maslahi ya Taifa
Akizungumza kwa nyakati tofauti alipokuwa kwenye ziara ya kamati ya utekelezaji kuzitembelea kata zote 21 za wilaya ya Namatumbo alisema kuwa suala la uzalendo kwa vijana ni suala muhimu na kusisitiza vijana hao kutokukubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kwa ajili ya kutimiza malengo yao ya kupata nafasi za uongozi na baadae kuwawacha vijana wakiwa hawajui la kufanya bila ya kuwasaidia katika kuwainua kiuchumi.
Luambano amewataka vijana wa kike kuacha kukubali kuolewa wakati wakiwa hwajamaliza shule kwani kufanya hivyo kutapelekea taifa kukosa viongozi bora wenye uzalendo na taifa lao.
“Viongozi wanaofanya kazi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo kuepuka kupikiana majungu na kufitiniana na badala yake wafanye kazi kwa kushirikiana pamoja kwa kuwashirikisha vingozi wa serikali na Chama katika ngazi za shina,tawi na kata wakitekeleza majukumu yao”alisema Luambano
Ameitaka jamii kuwapa uhuru vijana hasa wa kike kugombea nafasi za uongozi pamoja na kuzingatia maadili ya uongozi ili waweze kuwatumikia wananchi katika sekta mbalimbali na wao waepukane kutumiwa kwa ajili ya watu kupata faida.
Aliewaleza viongozi hao wa chama kwamba, wasisite kuitembelea na kuikaguwa miradi inayotekelezwa na serikali katika ngazi pamoja na kutoa maelekezo pale inapohitajika lengo likiwa ni kuhakikisha ahadi zilizotolewa na viongozi wakati wakiinadi ilani hiyo zinatakelezwa kwa vitendo.
Luambano alisema kuwa lengo la ziara ni kuimarisha Uhai wa jumuiya, Sambamba hivyo amezitaka kata zote kujiimarisha kiuchumi kwa kushiriki kilimo kwa msimu wa 2023/2024 ambapo kila kata imetakiwa kulima hekari zisizopungua 5 za zao lolote rafiki linalostawi katika eneo husika lakini pia kila tawi katika kata husika lishiriki kilimo kwa hekari zisizopungua 02.
Aidha Luambano amewahamasisha vijana wenye sifa kuunda vikundi vya ujasiriamali iliwaweze kukopesheka kwa lengo la kujiinulia kipato
Pia katika ziara hiyo ambayo ilianza agosti 17 na kumalizika agosti 25 mwaka huu Mwenyekiti aliongoza kamati ya utekelezaji kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo kamati hiyo ilitembelea eneo la kihistoria lililopo Kata ya Luegu , eneo ambalo alilala Baba wa taifa hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere akiwa katika harakati za kupigia uhuru mwaka 1955, ambapo lengo la kutembelea eneo hilo ni kulitangaza ili lifahamike katka historia ya Tanzania na vijana waweze kulifahamu kiufasaha.