Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza viongozi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida ambapo amesema kuwa maslahi ya watumishi ni kipaumbele katika awamu hii ya Sita ili kuongeza motisha na kuchochea zaidi utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa umma.
Sehemu ya wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya Unyamikumbi, Manispaa ya Singida amesema wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo amewaeleza kuwa Serikali imetoa zaidi ya bilioni 51 kwa ajili ya kunusuru kaya hizo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Taasi mbalimbali katika mkoa wa Singida pamoja na Wajumbe wa Kamari ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Singida wakimsiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akioneshwa ramani ya majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili mara baada ya kufika katika eneo hilo kwa ajili kukagua ujenzi wa chuo hicho unavyoendelea
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza mara bada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili mara baada ya kufika katika eneo hilo
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida ambayo tayari yameshakamilika
Mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya Unyamikumbi, Manispaa ya Singida, Mariamu Luguti ambaye amewezeshwa kufuga mbuzi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo ameishukuru Serikali kwa kumsaidia kuondokana kwenye lindi la umasikini
Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu, Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt. Ernest Mabonesho akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo amesema ujenzi umefikia asilimia 21wa Chuo cha Utumisi wa Umma Kampasi ya Singida
…………………..
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesisitiza kuwa maslahi ya watumishi ni kipaumbele katika awamu hii ya Sita ili kuongeza motisha na kuchochea zaidi utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa umma.
Mhe. Ridhiwani amesema na kusisitiza hayo tarehe leo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida katika ofisi hizo.
“Kila mara tunaona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitangaza kutoa haki na stahiki mbalimbali kwa watumishi wa umma, hivyo, kila mmoja wetu kwa nafasi yake anatakiwa pia kuwajibika ipasavyo ili kuleta ufanisi zaidi” ameongeza Mhe. Ridhiwani.
Aidha, amewakumbusha watumishi hao kutoka ofisini na kwenda kuwahudumia wananchi na kutatua changamoto zilizo ndani ya uwezo wao.
Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani ametembelea na kukagua ujenzi wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili inayohusu majengo ya madarasa na vyoo vya nje na kuelekeza viongozi kuhakikisha miundombinu ya watu wenye ulemavu inazingatiwa katika ujenzi huo.
“Chuo cha Utumishi wa Umma ni muhimu sana kwa kuwa kinaandaa watumishi wa umma bora na ambao ni msingi wa maendeleo ya nchi katika nyanja zote” ameongeza Mhe. Ridhiwani.
Vilevile, akiwa katika ziara ya kutembelea wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya Unyamikumbi, Manispaa ya Singida amesema Serikali imetoa zaidi ya bilioni 51 kwa ajili ya kunusuru kaya maskini nchini ili ziweze kuboresha maisha yao mathalani kwa kupata chakula milo 3 kwa siku, kusomesha watoto na kupata huduma za matibabu kwenye vituo vya afya na zahanati.
Naye, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Bw. Stanislaus Choaji amesema wamepokea maelekezo na watahakikisha wanatazama kwa jicho pevu maeneo ya pembezoni katika Mkoa wa Singida kwa kutoa na kupanga watumishi ili kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
Aidha, Bw. Choaji ameongeza kuwa wananchi wa Mkoa wa Singida wananufaika na uwepo wa TASAF kwa kuwa kaya maskini ambazo ni wanufaika wamepata fedha na wanafanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kufuga Mbuzi, Kuku na Kondoo kwa ajili ya kujikwamua katika wimbi la umaskini, hivyo salamu za shukurani zimfikie Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ukombozi huo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu, Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt. Ernest Mabonesho amesema ujenzi umefikia asilimia 21 na kazi inayoendelea ni ujenzi wa kuta ambapo hadi sasa mradi huo umetoa ajira za vibarua kwa wananchi 96 wanaozunguka eneo la mradi ikiwa wanaume ni 62 na wanawake ni 34.
Mhe. Ridhiwani amehitimisha ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Singida ambapo alianzia Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kumalizia katika Manispaa ya Singida. Ziara hiyo ililenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa huo.