Na Julieth Laizer ,Arusha
Ushirika wa Wachungaji wa Kipentekoste Tanzania(PPFT) wanamuunga mkono Rais Samia Hassan Suluhu kwa kauli yake ya kutamka na kufunga mjadala wa bandari
Aidha baada ya Rais kutamka kunyamaza kimya wanamuomba afunge mjadala huo badala yake wale watakaoendelea kuongea baada ya Rais kutamka wachukuliwe hatua.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Arusha, Mwenyekiti wa PPF Taifa,Askofu Ikongo alisema kila mmoja ametoa maoni kuhusu suala la bandari na endapo kunakasoro katika mkataba huo zirekebishwe Kwa maslahi ya nchi.
Alimpongeza Rais Samia kwa kutoa kauli ya kunyamaza kimya lakini aliongeza
kwa kusema kuwa kunyamaza kimya huko kunatoa nafasi ya watu wengine kuendelea kujadili ilhali suala hilo limejadiliwa sana basi ifike ukomo wake
“Rais anaponyamaza utulivu unakuwepo na kila mtu ameongea lakini kwasababu Rais ametoa nafasi sipingani nao lakini sasa Rais atamke kwakusema sasa basi amepokea maoni ya kila aliyesema kuhusu bandari sasa iwe mwisho”
Alisema ni vema sasa mjadala ya bandari ufungwe hivyo alimuomba Rais afunge mjadala huo kuonana na Rais kwaajili ya
Alisisitiza kuwa endapo Rais atafunga mjadala huo watakaoendelea kuongea au kuhamasisha maandamano watachukulia hatua zitakzostahiki na wale watakaofanya maandamano ya amani ambayo ni shinikizo na kunatofauti kubwa kati ya maandamano ya amani na kutoa maoni.
Mwisho