Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (katikati) na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (kulia) wakimsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kwanza kushoto) wakati wa kikao cha Msajili na chama cha CHADEMA chenye lengo la kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na ORPP)
Mwenyekiti wa CHADEMA meshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kushoto), akisisitiza jambo mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, wakati wa kikao cha Msajili na viongozi waandamizi wa CHADEMA leo jijini Dar es Salaam. Kikao cha Msajili na CHADEMA ni juhudi za ofisi hiyo kuimarisha hali ya kisiasa hususan demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini. (Picha na ORPP).
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Jaji Mutungi amekutana na viongozi hao leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni muda mrefu umepita viongozi hao wakiwa hawajakutana na kuonekana kwenye jamii.
Msajili katika kikao hicho amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Aikael Mbowe, Katibu Mkuu John Mnyika na Katibu wa Baraza la Wazee (BAZECHA) ndugu Rodrick Rutembeka.
Kwa upande wa Msajili walikuwepo Naibu Msajili Mohamed Mohamed na Ofisa wa Ofisi hiyo Sisty Nyahoza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo kikao kilikuwa na lengo la kuimarisha mazingira ya siasa hususani demokrasia ya vyama vingi vya siasa.