Na Sophia Kingimali
KUFUATIA juhudi zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha sekta ya kilimo na kuvutia uwekezaji) katika sekta hiyo, Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa jukwaa la mifumo ya chakula (AGRF) linatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam Septemba 5 mpaka 8 , 2023
Akizungumzia maandalizi ya Kongamano hilo mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathmini Bw. Joseph Kiraiya amesema ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano huo umekuoa wa tofauti na miaka ya nyuma kwani mwanzo ilikua kwa kuchangiliwa lakini Sasa wenyeji wa mkutano huo imetokana na kushindanishwa na nchi nyingine.
“Mafanikio tunayoyaona Sasa katika wizara ya kilimo ni kutokana na jitahada zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya kilimo hivyo mapinduzi makubwa yaliyofanyika yanatoa matokeo chanya Kwa taifa”amesema Kiraiya
Aidha Kiraiya amesema kuwa jukwaa la mifumo ya chakula itatoa fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya kilimo hivyo taasisi na sekta binafsi zinapaswa kujisajili ili kushiriki katika katika mkutano huo ambao unatarajiwa kushirikisha marais na wakuu wa nchi mbalimbali Duniani.
Amesema matarajio ya mkutano huo ni kukuza sekta ya utalii Kwani kutakua na utalii wa kilimo ambapo wageni watatembelea maeneo mbalimbali ili kujionea uzalishaji unaofanywa nchini.
Aidha Kiraiya ameongeza kuwa mkutano huo utaongeza ajira Kwa vijana na kukuza uchumi kwa Taifa lakini pia kukuza biashara na kuhamasisha uwekezaji..
“Mageuzi ya sekta ya kilimo yataletwa na vijana na wanawake hivyo jukwaa hili ni fursa kwa kila mmoja wetu kuitumia ili kukuza kipato na kuinua uchumi wa nchi yetu”ameongeza Kiraiya
Sambamba na hayo mkutano huo unatarajiwa kushirikisha wakuu wa nchi ambapo mpaka Sasa wizara ya kilimo imetoa mialiko Kwa Marais 17 na mawaziri wanohusika na maswala ya kilimo na uvuvi 43 lakini washiriki waliojisajili mpaka Sasa ni 23000 huku lengo likiwa kuwa na washiriki 3000.
Akizungumzia maandalizi Kiraiya amesema kuwa mpaka Sasa maandalizi yote muhimu yameshakamilika ikiwemo maeneo watakayofikia wageni pamoja na sehemu za vivutio watakavuotembelea.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Nyerere JNICC jijini Dar es salaam September 5 mpaka 8.