Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH
Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) Anandumi Mmari akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kilalo Barati akimpima shinikizo la damu mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana
…………………………
Na: Mwandishi Maalum – Kilimanjaro
Wananchi zaidi ya 7000 wafikiwa na huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo kupitia huduma ya tiba mkoba ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge leo wakati akifungua kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayoendelea mkoani Kilimanjaro katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH).
Dkt. Kisenge alisema JKCI imekuwa ikifanya huduma ya tiba mkoba katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo hadi sasa mikoa 11 ya Tanzania bara na Zanzibar imeshafikiwa na wananchi takribani 700 kupewa rufaa kufika JKCI kwa ajili ya matibabu zaidi.
Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema kambi hiyo ya matibabu ya moyo ni muendelezo wa tiba mkoba ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services yenye nia ya kuwafikishia wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro huduma ya tiba bobezi ya magonjwa ya moyo mahali walipo.
“Nia ya JKCI kufanya kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi ni kuhakikisha kuwa tunaendeleza ujuzi kwa wataalamu wa afya wa hapa Mawenzi pamoja na kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao wana magonjwa ya moyo”,
“Mwitikio katika Mkoa huu wa Kilimanjaro umekuwa mkubwa sana ndani ya siku mbili tayari wagonjwa 600 wamefika katika Hospitali hii kwa ajili ya kupatiwa huduma, wagonjwa wengi wanaofika tumewakuta na shinikizo la damu na hii inatokea katika kila mkoa tunaoenda ugonjwa wa shinikizo la juu la damu umekuwa changamoto kwa watu wengi hivyo kupata madhara ya moyo kutanuka”,