Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Godrefy Chongolo, amekutana kwa ajili ya mazungumzo na Kansela wa Chama Cha Kikomunisti Cha China (CPC) katika Ubalozi wa China nchini Tanzania Ndugu Xu Sujiang pamoja na Kansela wa Uchumi na Biashara wa ubalozi huo, Chu Kun, leo Jumanne, Agosti 22, 2023, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es salaaam.