RC Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amepongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Amir Mkalipa kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo pia amepongeza wananchi wa Kata ya Muungano Tarafa ya Masama Wilayani Hai kwa kujitoa katika kuchangia miradi inayoendelea katika maeneo yao.
Ameyasema hayo Mhe. Babu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi Mlima Shabaha yenye jumla ya vyumba tisa vya madarasa, jengo la utawala,matundu kumi na sita ya vyoo pamoja na kichomea taka inayotekelezwa na Mradi BOOST na umegharimu kiasi cha Tshs. 348,500,000.00
Naye Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Amir Mkalipa amesema shule hiyo inaenda kuwa mkombozi wa wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu zaidi ya Km.2 kufuata elimu na pia itawalinda wanafunzi wasifanyiwe vitendo viovu na wapita njia wanapokuwa njiani.
Hata hivyo Mhe. Mkalipa ametoa pongezi zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Fedha nyingi za miradi katika Wilaya hiyo.