Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.Stergomena Tax akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 21, 2023.
……………………..
Na Sophia Kingimali
Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo anatarajia kuwasili leo Agosti 21 jioni nchi kwaajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili ili kuendeleza uhusiano baina ya nchi hizo mbili uliohasisiwa na waasisi wake.
Akizungumza leo Agosti 21 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.Stergomena Tax amesema rais huyo anatarajiwa kupokelewa na Rais Samia Suluhu Hassani na kufanya mazungumzo ikulu ya Magogoni Dar es salaam ikiwa pamoja na kutiliana sain ya mikataba ya ushirikiano baina ya nchi hizo.
“Ziara hii ni kazi kubwa anayoifanya Rais Samia Suluhu Hassani kuinganisha nchi na mataifa mbalimbali”amesema Tax.
Amesema hati ya makubaliano watakayosaini italenga katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Nishati,madini,uchumi wa bluu,ushirikiano wa kimataifa uhamiaji na biashara.
Aidha Tax ameongeza kuwa Tanzania na Indonesia zinaushirikiano wa kidiplomasia wa muda mrefu ambao uliasisiwa na mwalim Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Indonesia Soekamo mnamo mwaka 1964.
Amesema katika ushirikiano huo wamefanikiwa kwatika uwekazaji ambapo Hadi kufikia mwaka 2023 Indonesia imewekeza katika miradi mitano katika sekta ya kilimo,uzalishaji viwandani na ujenzi.
Ziara ya Rais Widodo ni ziara ya pili Kwa kiongozi wa nchi hiyo kutembelea nchini ambapo ziara ya kwanza ilifanywa na Rais wa pili wa nchi hiyo Soeharto disemba 5,1991 ikiwa ni miaka 32 imepita
Chimbuko la uhusiano huo ni mkutano uliofanyika Bandung 1925 ambapo nchi nyingi za Afrika zilikua chini ya utawala wa kikoloni.