Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamadi akimkabidhi albamu ya tungo njema Sheha wa shehia ya Pongwe Pwani Fatma Faki kwaniaba ya mkuu WA wilaya ya Kati Marina Tomas wakati wa Hafla ya chakula kwaajili ya mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambaya hufanyika Kila mwisho WA mwezi wa septemba kwa Kila mwaka.
Mkurugenzi wa Redio Al-nuor Ali Mkubwa Zubeir akizungumza na wadau wa tungo njema kabla ya kumkaribisha kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Khamis Hamad Khamis kuzungumza na hao wakati wa Hafla ya chakula kwaajili ya mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa Septemba hafla iliyofanyika viwanja vya Skuli ya Pongwe Pwani.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamadi akizungumza na wadau wa tungo njema wakati wa Hafla ya chakula kwa watoto yatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa septemba Urowa.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Khamis Hamad Khamis (alievaa kanzu) akiwa katika PICHA ya pamoja na Kijana Abdillah mwenye ulemavu wa uoni mwenye kipaji cha kusoma nasheed katika hafla ya chakula kwaajili ya watoto mayatima iliyofanyika Uroa Pongwe Pwani.
Wanafunzi wa Pongwe Pwani wakisoma utenzi wenye maudhui ya kuwaenzi mayatima katika Hafla ya chakula kwaajili ya mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa septemba.
Wanafunzi wa Skuli ya Dkt Samia wakisoma utenzi wenye maudhui ya kuwatunza mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa septemba ,hafla iliyofanyika urowa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Wasanii wa mashairi Zero kasorobo na daktari wa mashairi wakitoa burudani ya shairi lenye maudhui ya kuwatunza mayatima katika Hafla ya chakula kwaajili ya mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa septemba
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad akimkabidhi misahafu Mkurugenzi wa Redio Al-nuor Ali Mkubwa Zubeir kwa niaba ya watoto mayatima wakati wa chakula cha mchana ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila ifikapo mwisho wa mwezi wa 9.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad akiwa na watoto yatima katika chakula cha pamoja kilichoandaliwa na wadau wa mashairi ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa 9,hafla iliyofanyika Viwanja vya Skuli ya Pongwe Pwani.
……
Na fauzia Mussa
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema jamii ya wazanzibari ipo pamoja na watoto mayatima na itaendelea kuwajali ili na wao wajisikie kama watoto wengine.
Akizungumza na wadau wa tungo njema katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Redio Al-Nour kwa watoto hao huko viwanja vya Skuli ya Pongwe Pwani , kamishna Hamadi alisema mjumuiko huo umeonesha upendo na kuwatia moyo katika safari yao ya maisha.
Sambamba na hayo Alizitaka TAASISI mbalimbali kujitokeza kutoa nyenzo zinazohitajika,fursa na mifumo ya usaidizi ili kuhakikisha watoto hao wanafikia malengo.