Awali wakieleza kuhusu makundi hatarishi ambayo nguvu zaidi inahitajika kuwekezwa ili kukabiliana na maradhi ya VVU na Ukimwi na kisha kufikia mpango wa Tisini na tano tatu wadau akiwemo Enock Mgaya ambaye ni dereva bodaboda wametaja kundi la Wavuvi,Magereza,Walemavu pamoja na madereve wa masafa marefu kuwa ni sehemu zinazohitaji elimu kubwa juu ya ugonjwa huo ili kuhamasisha kupima afya na kisha kuanza matumizi ya dawa za kufubaza virus
Mbali na kuainisha makundi hayo,Katika mdahalo huo kundi la bodaboda limeonekana kuhitaji elimu zaidi ya ugonjwa huo kwa kuwa baadhi ya madereva wamekuwa wakituhumiwa kuwabaka wateja wao wakike wanapowasafirisha usiku wakiwa wamelewa jambo ambalo linaweza kusababisha kupata maambukizi.
“Kundi hili la bodaboda linahitaji kupata elimu ya kutosha kwasababu kuna madereza bodaboda wanapobeba wateja wakike usiku wakiwa wamelewa huwalazimisha mapenzi bila kuchukua tahadhali zozote ,Hivyo mimi baada ya kupata elimu hii nitajitahidi kwenda kuelimisha wenzangu,alisema Enock Mgaya dereva bodaboda”
Kundi lingine ambalo linadaiwa kukwamisha jitihada za serikali na wadau katika kufikia 95 tatu ni pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ambao wamedaiwa kuaminisha waumini wao kwamba maombi yanaweza kuponya maradhi hayo jambo ambalo linapingwa vikali na wadau na kisha kutoa ushauri kupitia mdahalo huo kwenda kuwachukulia hatua watumishi hao.
Kwa upande wao viongozi wa dini akiwemo Amon Mwakipesile Mwakilishi wa Bwakwata NJOMBE na Padre Elias Msemwa wamesema elimu iongozwe kwa jamii juu ya maradhi hayo na kisha kusema kwamba kinachofanywa na baadhi ya viongozi wa dini kinapaswa kukemewa vikali kwasababu suala la ugonjwa linahitaji dawa na sio maombi.
Wamesema viongozi wa dini wanapaswa kuelimisha waumini kupima afya na pindi wanapobainika kuwa na maambukizi waanze kutumia dawa ili kunusuru na vifo vinavyoweza kuzuilika .
Licha ya changamoto zinazokwamisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi lakini ratibu wa ukimwi halmashauri ya mji wa Njombe Daniel Mwasongwe amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kuzikia 95 zote tatu na kisha kusema kwamba mikakati iliyowekwa inakdwenda kuwafikia kwa ufanisi mkubwa kundi la vijana wenye umri wa kuanizia miaka 14 hadi 19 ambalo linaonekana kutofikiwa ipasavyo katika mapambano hayo.
Mara baada ya kupokea mapendekezo na mikakati ya kuyafikia kwa ufanisi makundi tajwa ili kufikia malengo ya 2030 ndiyo Japhet Kakwezi kutoka mradi wahebu tuyajenge akasema anachukua mikakati hiyo na kwenda kuiwasilisha katika ngazi ya kitaifa ili iweze kufanyika