Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Ng’wilabuzu Ludigija mwenye (Tisheti Ya blue) akiwa na wadau mbalimbali wa elimu wakitembelea shule ya sekondari Mwamashimba.
Wanafunzi wa kidato cha Tano.
………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkuu wa wilaya ya Kwimba Ng’wilabuzu Ludigija amewataka wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za sekondari zilizopo katika wilaya hiyo kuripoti katika shule zao ili waanze kupata elimu baada ya serikali kukamilisha maiundombinu ya madarasa, vyoo na mabweni.
Ludigija amesema nafasi zao zipo na kama kuna wengine wanataka kuhamia katika shule hizo za Mwamashimba, Sumve, Talo na Ngudu wanakaribishwa huku akimshukuru Rais Dkt Samia kwa kutoa fedha za kuboresha na kujenga miundombinu katika shule hizo ili wanafunzi wapate mazingira mazuri ya kujisomea.
Amesema tangu shule zilipofunguliwa hadi leo hii wanafunzi wanaendelea kuripoti na kwamba ataendelea kutembelea shule hizo ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti.
‘naendelea kusema kwa wananchi hasa wazazi waendelee kuwaleta shuleni watoto wao na shule zote za kidato cha tano tumejipanga kwa miundombinu ya kutosha waje tu hapa tunawasubiri na vitanda vipo vya kutosha hadi vinabaki, Rais amefanya mapinduzi makubwa sana kwenye miundombinu ya kujifunzia pamoja na madarasa na shule za kwimba ni moja kati ya shule zinanofanya vizuri sana”, amesema
Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya sekondari Mwamashimba akiwemo Hamisa Saidi na Ana Ayoub wakamuahidi mkuu huyo wa wilaya kufanya vizuri katika masomo yao ili warudishe fadhila kwa Rais Samia kwa jinsi alivyowawekea mazingira mazuri ya kujisomea.
‘Tunapenda kumshukuru sana Rais Samia kwa kutusaidia tulipofika hapa shuleni tukaona madarasa mabweni na vyoo vizuri tunamuahidi kufaulu vizuri sana na tutapata division one nyingi”,wamesema